Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Balozi mpya wa Misri
hapa nchini Mhe. Mohamed Gaber Mohamed Abulwafa (kushoto) aliyefika
ofisini kwa Makamu wa Rais kwa lengo la kujitambulisha, Ikulu jijini Dar
es Salaam (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na
Balozi mpya wa Misri hapa nchini Mhe. Mohamed Gaber Mohamed Abulwafa
(kushoto) mara baada ya kumaliza mazungumzo ofisini kwa Makamu wa Rais,
Ikulu jijini Dar es Salaam (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Balozi mpya wa Spain
nchini Mhe. Francisca (kushoto) aliyefika kujitambulisha ofisini kwa
Makamu wa Rais, Ikulu jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa
Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na
Balozi mpya wa Spain nchini Mhe. Francisca Pedros (kushoto) mara baada
ya kumaliza mazungumzo ofisini kwa Makamu wa Rais, Ikulu jijini Dar es
Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiagana na Balozi mpya wa Spain
nchini Mhe. Francisca Pedros(kushoto) mara baada ya kumaliza mazungumzo
ofisini kwa Makamu wa Rais, Ikulu jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi
ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Balozi mpya wa
Ethiopia nchini Mhe. Yonas Yosef Sanbe aliyefika kujitambulisha leo
Ofisini kwa Makamu wa Rais, Ikulu jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi
ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na
Balozi mpya wa Ethiopia nchini Mhe. Yonas Yosef Sanbe aliyefika
kujitambulisha leo Ofisini kwa Makamu wa Rais, Ikulu jijini Dar es
Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
………………………..
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo tarehe 31 Januari, 2019 amekutana
na kufanya mazungumzo na Mabalozi kutoka nchi 3 ofisini kwake jijini Dar
es Salaam.
Balozi wa kwanza kukutana na Makamu wa
Rais, alikuwa Mhe. Gaber Mohamed Abulwafa Balozi mpya wa Misri hapa
nchini ambaye alifika kwa lengo la kujitambulisha na pia kuzungumzia
mambo
mbali mbali ya kuimarisha uhusiano baina ya nchini mbili ambao
ulianzishwa na waliokuwa marais wa nchi hizi, Baba wa Taifa Hayati
Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Rais Gamal Abdel Nasser Hussein wa
Misri.
“Misri itaendelea kutoa ushirikiano katika
masuala ya Elimu, Afya na masuala ya teknolojia ya ujenzi wa
miundombinu yenye tija kwa mataifa haya mawili” alisema Balozi huyo.
Mwisho Balozi huyo mpya wa Misri aliahidi kusimamia miradi yote ambayo ipo kwenye makubaliano baina ya Serikali hizi.
Kwa upande wake Makamu wa Rais alimpongeza
na kumkaribisha Tanzania pamoja na kumhakikishia ushirikiano mzuri
katika kazi zake akiwa hapa nchini na kumueleza kuwa kwa miaka mingi
uhusiano kati ya Misri na Tanzania umezidi kuimarika.
Balozi wa Pili kukutana na kuzungumza na
Makamu wa Rais alikuwa Mhe. Francisca Pedros, Balozi mpya wa Spain hapa
nchini ambaye Makamu wa Rais alimpongeza kwa kuwa Balozi wa kwanza
mwanamke kuteuliwa kuja kuitumikia nchi yake hapa nchini.
Balozi wa Tatu kukutana na kufanya
mazungumzo na Mheshimiwa Makamu wa Rais ni Balozi wa Ethiopia nchini
Mhe. Yonas Yosef Sanbe ambaye alimueleza Makamu wa Rais furaha yake ya
kuwa hapa na kuona namna mahusiano ya nchi hizi mbili yameboreka ambapo
alisema kuwa
“nafarijika kuona namna ambavyo wanawake wanapewa nafasi za juu katika uongozi katika nchi hizi mbili”
Makamu wa Rais pamoja na mambo mengine
alimpongeza Balozi huyo wa Ethiopia kwa kuwa Balozi wa kwanza mwenye
makazi yake hapa Tanzania.
No comments :
Post a Comment