Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa leo
Novemba 3, 2018, amefunga wiki ya maonesho ya viwanda Kibaha, Mkoani
POwani, yaliyokuwa yakifanyika kwenye viwanja vya CCM-Sabasaba, eneo la
Picha ya Ndege.
Moanesho
hayo yaliyofunguliwa na Makamu wa Rais, Mhe. Samia Suluhu Hassan,
Oktoba 29, 2018, yalilenga kuwakutanisha wazalishaji bidhaa za wviwanda
na wanunuzi (masoko), ambapo pia taasisi za serikali zinazohusika na
utoaji huduma mbalimbali zilishiriki pia.
Miongoni
mwa taasisi hizo, ni Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi WCF, ambao kazi
yake kubwa ni kutoa Fidia kwa wafanyaklazi walioumia, kuugua au kufariki
kutokana na kazi.
Moja ya ujumbe mkubwa alioutoa siku anafungua maonesho hayo kwa waajiri kote nchini, Makamu wa Rais aliuagiza
uongozi wa (WCF), kuendelea
kuwafuatilia waajiri ambao bado hawajajisajili ili waweze kufanya hivyo.
Makamu wa Rais alitoa wito huo leo Oktoba 29,
2018 alipotembelea banda la Mfuko huo kwenye maonesho ya viwanda Mkoa wa Pwani
kwenye viwanja vya CCM-Sabasaba, Picha ya Ndege Mkoani humo.
Alisema
viwanda vimeongezeka nchini na kwamba
huduma za WCF zitahitajika sana kwa wakati huu na hivyo kuutaka uongozi
wa
Mfuko, kuhakikisha unaendelea na ufuatiliaji kwa waajiri wa zamani na
wapya ambao bado hawajajisajili na kuwasilisha michango kwenye Mfuko
watekeleze takwa hilo la kisheria ili
mfanyakazi anapoumia aweze kupata haki yake ya fidia.
“Waajiri wao muwabane wajisajili na mfuko na
waweze kuwasilisha michango ili Mfuko uendelee kuwa na uwezo wa kulipa fidia,
pale watoto wetu (wafanyakazi) wanapokatika vidole au kuumia waweze kupata
haki zao.” Alisisitiza.
Katika
hatua ya kuimarisha Hifadhi ya Jamii, Tanzania, Serikali ilianzisha Mfuko wa
Fidia Kwa Wafanyakazi kwa mujibu wa kifungu namba 5 cha sheria ya Fidia kwa
Wafanyakazi, kipengele cha 263 kilichofanyiwa marejeo mwaka
2015 ili kuhakikisha kila mfanyakazi Tanzania Bara kutoka sekta ya umma na
binafsi anapata fursa ya kuwekewa bima na mwajiri wake ili anapopata majeraha
au magonjwa awapo kazini basi aweze kufidiwa kwa mujibu wa sharia.
WIZARA, MIKOA ONDOENI VIKWAZO UJENZI WA VIWANDA-MAJALIWA
NA OWM, PWANI
WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amezitaka Wizara zinazohusika na masuala ya
viwanda, Ofisi za Wakuu wa Mikoa, Wilaya na Mamlaka za Serikali za Mitaa
pamoja na sekta binafsi watambue na waondoe vikwazo na urasimu dhidi ya
ujenzi na ustawi wa viwanda nchini.
Pia, Waziri Mkuu amemuagiza Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji,
Charles Mwijage ampelekee taarifa ya hatua iliyofikiwa juu ya kampuni ya
Budget Motors walioomba kibali cha kutengeneza na kuunganisha bodi za
mabasi tangu mwaka jana na hawajajibiwa.
Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo (Jumamosi, Novemba 3, 2018) wakati
akifunga wiki ya maonesho ya viwanda yaliyofanyika kwenye Viwanja vya
Sabasaba katika kata ya Picha ya Ndege, Kibaha mkoani Pwani. Amesena
uwepo wa viwanda nchini unatoa ajira nyingi.
“Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli
imeamua kujenga uchumi wa viwanda utakaokuwa mhimili mkuu wa maendeleo
ya Taifa na wananchi, hivyo itaendelea kutoa ushirikiano ili kuhakikisha
ajenda ya ujenzi wa viwanda inafanikiwa.”
Amesema katika kupunguza vikwazo na kuboresha sera nchini, Rais Dkt.
Magufuli ameweka msukumo wa kutosha ili kurahisisha na kuondoa
ukiritimba kwenye shughuli zote za kibiashara, lakini pia katika
kuboresha sera za Taifa za kodi ili kulinda viwanda vya ndani
Waziri Mkuu amesema umuhimu wa viwanda umetokana na Ilani ya uchaguzi ya
Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka 2015/2020 ambayo inaielekeza
Serikali kuweka nguvu katika ujenzi wa viwanda ili kufikia malengo ya
Dira ya Maendeleo ya Taifa ya mwaka 2025.
Amesema kwa msingi huo, Rais Dkt. Magufuli alitoa msukumo wa sekta
binafsi nchini kuanzisha viwanda vinavyotumia malighafi zinazozalishwa
nchini kutokana na mazao ya kilimo, mifugo, uvuvi na maliasili, vikiwemo
viwanda vya nguo, sabuni, korosho na matunda.
Waziri Mkuu ameongeza kuwa uwepo wa viwanda nchini utasaidia kuongeza
wigo wa mapato ya Serikali kupitia kodi na tozo mbalimbali. “Huu ndio
mwelekeo wa Serikali ya awamu ya tano unaolenga kuifikisha nchi kwenye
uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.”
Kuhusu suala la kampuni ya Budget Motors, Wiziri Mkuu amesema ifikapo
Ijimaa (Novemba 9, 2018) Waziri wa Viwanda Biashara na Uwekezaji
awasilishe taarifa kuhusu suala hilo la kibali. “Huu ni urasimu, ni bora
apewe atengeneze na akikosea arekebishwe.”
Kampuni ya Budget Motors inadai kuwa iliomba kibali cha kuwa na
uthibitisho wa kutengeneza na kuunganisha bodi za mabasi kutoka Shirika
la Viwango Tanzania (TBS), kwa takribani mwaka mmoja bila ya kujibiwa.
Walitoa malalamiko hayo kwa Waziri Mkuu alipotembelea banda lao.
Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu ametoa rai kwa taasisi zenye
miradi mbalimbali nchini pamoja na wananchi kuthamini na kuzitumia
bidhaa zinazozalishwa na viwanda vya hapa nchini zikiwemo na za viwanda
vya mkoa wa Pwani kwani zina viwango vya ubora.
“Wakati natembelea mabanda kwenye maonesho haya nimeshuhudia bidhaa
nyingi nzuri na zenye ubora. Nimeona wazalishaji wa saruji, mabati,
nondo, marumaru, mabomba ya plastiki, chuma, zana za kilimo, vyakula,
vinywaji na vifungashio.”
Waziri Mkuu amesema kupitia maonesho hayo ya viwanda vilivyopo katika
mkoa wa Pwani vimeudhihirishia umma kuwa vina uwezo mkubwa wa kuzalisha
bidhaa zilizo bora na hata kuzidi zile zinazoingizwa kutoka nje,
amewahamasisha wananchi kutumia bidhaa za ndani.
Kwa upande wake, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Selemani
Jafo ameiagiza mikoa yote nchini kuhakikisha inatumia bidhaa
zinatengenezwa na viwanda vya ndani katika miradi mbalimbali ya ujenzi
wanayoitekeleza kama ujenzi wa hospitali za wilaya na vituo vya afya.
Amesema Wakuu wa Mikoa ni lazima wahakikishe bidhaa kama saruji, nondo,
marumaru, mabati zinavyotumika katika ujenzi ziwe vimezalishwa na
viwanda vya ndani kwa sababu vina viwango vya ubora unaotakiwa na pia
itasaidia kuondoa tatizo la soko la bidhaa hizo.
Naye,Waziri Mwijage amewataka watendaji wanaohusika na masuala ya
viwanda kutoweka vikwazo kwa wawekezaji ambao wanakwenda katika ofisi
zao kwa ajili ya kutafuta maeneo ya kuwekeza kwenye viwanda au
wanaohitaji vibali kwani jambo hilo halina tija.
| Mkurugenzi wa Uendeshaji, Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Bw. Anselim Peter(kulia), akimsikilzia mwananchi huyo aliyetembelea banda la Mfuko aliyetaka kujua kazi za Mfuko huo. |
| Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa akiungana na vijana wa bendi ya muziki wa dansi ya kambi ya JKT-Ruvu walipotumbuiza wakati wa hafla hiyo ya ufungaji maonesho ya viwanda Kibaha leo Novemba 3, 2018. |
| Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa akiungana na vijana wa bendi ya muziki wa dansi ya kambi ya JKT-Ruvu walipotumbuiza wakati wa hafla hiyo ya ufungaji maonesho ya viwanda Kibaha leo Novemba 3, 2018. |

No comments :
Post a Comment