Friday, November 2, 2018

WADAU WA SEKTA YA UJENZI WAKUTANA KUJADILI MAREKEBISHO YA SHERIA YA BARAZA LA TAIFA LA UJENZI


????????????????????????????????????
Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Mipango kutoka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Bi. Elizabeth Tagora, akifungua mkutano wa wadau wa Sekta ya Ujenzi kujadili mapendekezo ya marekebisho ya sheria ya Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC) ili kuimarisha na kuhuisha baraza hilo. Mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC), jijini Dar es Salaam.
????????????????????????????????????
Mtendaji Mkuu wa Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC), Dkt. Matiko Mturi, akizungumza na wadau mbalimbali wa Sekta ya Ujenzi (hawapo pichani), waliohudhuria mkutano wa kujadili mapendekezo ya marekebisho ya sheria ya baraza hilo, jijini Dar es Salaam.
3a
3b
Wadau  mbalimbali kutoka Sekta za Ujenzi hapa nchini waliohudhuria mkutano wa kujadili mapendekezo ya marekebisho ya sheria ya Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC), wakimsikiliza Mtendaji Mkuu wa baraza hilo Dkt. Matiko Mturi (hayupo pichani), katika mkutano uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC), jijini Dar es Salaam.
????????????????????????????????????
Picha ya pamoja ya wadau wa sekta ya ujenzi waliokutana kujadili mapendekezo ya marekebisho ya sheria ya Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC), ili kuimarisha na kuhuisha baraza hilo.

No comments :

Post a Comment