Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la reli Tanzania
(TRC), Masanja Kadogosa kuhusu ujenzi wa Reli ya SGR wakati
alipotembelea kambi ya Kampuni ya Yapi Markezi inayojenga Reli hiyo,
katika eneo la Shaurimoyo jijini Dar es salaam, Novemba 3, 3018.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akikagua maandalizi ya ujenzi wa madaraja ya kupitisha treni juu
wakati alipotembelea kambi ya Kampuni ya Yapi Merkezi inayojenga reli
ya Kisasa ya SGR Oktoba 3, 2018. Kambi hiyo ipo eneo la Shaurimoyo
jijini Dar es salaam. Wapili kushoto ni Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano, Mhandisi, Isack Kamwelwe.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akikagua kazi ya utengenezaji mataluma ya reli ya SGR wakati
alipotembelea Kambi ya Kampuni ya Yapi Merkezi katika eneo la Soga
mkoani Pwani, Oktoba 3, 2018. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi
Evarest Ndikilo.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akikagua utandikaji wa reli ya SGR katika eneo la Soga mkoani Pwani,
Oktoba 3, 2018. Wapili kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli
Tanzania (TRC), Masanja Kadogosa.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akikagua utandikaji wa Reli ya SGR katika eneo la Soga mkoani Pwani,
Oktoba 3, 2018. Kulia ni Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano,
Mhandisi, Isack Kamwelwe.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akikagua utandikaji wa Reli ya kisasa ya SGR katika eneo la Soga
mkoani Pwani, Oktoba 3, 2018. Kulia ni Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano, Mhandisi, Isack Kamwelwe na kulia kwa Waziri Mkuu ni
Mkurugenzi Mkuu wa Shiraki la Reli Tanzania (TRC), Masanja Kadogosa
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akiagana na wafanyakazi wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) pamoja na
wafanyakazi wa Kampuni ya Yapi Merkezi inayojenga reli ya kisasa ya SGR
kati ya Dar es slaam na Morogoro baada ya kukagua ujenzi wa reli hiyo
katika eneo la Soga mkoani Pwani, Oktoba 3, 2018. Kushoto ni
Mkurugenzi Mkuu wa TRC, Masanja Kadogosa. (Picha na Ofisi ya Waziri
Mkuu)
…………………………
*Ni baada ya kuhakikishiwa kipande Dar-Morogoro kitakamilika Aprili 2019 badala ya Julai
WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa
amesema ameridhishwa na kasi na viwango vya ujenzi wa
mfumo wa reli ya
kisasa (SGR) inayojengwa na kampuni ya Yapi Merkezi.
Amesema kipande cha kutoka Dar es
Salaam hadi Morogoro chenye urefu wa km. 300 ambacho kilitakiwa
kukamilika Julai 2019, wataalamu wamesema watakamilisha Aprili 2019.
Waziri Mkuu ameyasema hayo leo
(Jumamosi, Novemba 3, 2018) alipotembelea mradi wa ujenzi wa reli ya
kisasa kuanzia eneo la Shaurimoyo Dar esSalaam hadi Soga, Pwani.
“Nimeridhishwa na viwango na
maendeleo ya ujenzi kwa sehemu ulivyofikia pamoja na ushiriki wa
Watanzania wengi katika mradi huu, tunataka muendelee kujenga kwa kasi
hii.”
Waziri Mkuu amesema Serikali
inataka kuona malengo ya Rais Dkt. John Magufuli ya kutaka kuona
SGR inakamilika na kuanza kutumika nchini yanatimia.
Kuhusu suala la ajira, Waziri Mkuu
amesema amefarijika kusikia asilimia 96 ya watu walioajiriwa katika
mradi huo ni Watanzania, amewataka wawe mabalozi wazuri.
“Watanzania mnaofanya kazi katika
mradi huu hakikisheni mnawajibika kwa kufanyakazi kwa bidii, uaminifu na
muwe mabalozi wazuri ili wengine waweze wapate ajira.”
Awali,Mkurugenzi Mkuu wa Shirika
la Reli Tanzania (TRC), Masanja Kadogosa alisema awamu ya kwanza ya
mradi huo wa reli kutoka Dar es Salaam hadi Makutupora unagharimu sh.
trilioni 7.1.
Alisema mradi wa ujenzi wa reli
hiyo yenye urefu wa km 1,219 kutoka Dar es Salaam hadi Mwanza
umegawanyika katika vipande vitano, kipande cha kwanza ni kutoka Dar es
Salaam hadi Morogoro chenye urefu km 300 na kitagharimu sh. trilioni
2.7.
“Kipande kingine ni kutoka
Morogoro hadi Makutupora chenye urefu wa km. 422 ambacho kitagharimu sh.
trilioni 4.4, Makutupora hadi Tabora km. 376.5, Tabora hadi Isaka km
162.5 na Isaka hadi Mwanza km. 311.25.”
Mkurugenzi huyo alisema kukamilika
kwa reli hiyo ya kisasa kutachochea mipango ya Serikali katika
kutekeleza sera ya viwanda na kulifikisha Taifa kwenye uchumi wa kati
ifikapo mwaka 2025.
Pia reli hiyo itachochea mapinduzi
ya kiuchumi kwa kanda nzima ya Afrika Mashariki na Kati hususan kwa
nchi zisizopakana na bahari kwani watasafirisha mizigo yao kwa haraka na
uhakika.
Akizungumzia mradi huo kwa ujumla,
Kadogosa alisema maendeleo ya mradi huo ni asilimia 32 kwa kipande cha
Dar es Salaam-Morogoro na asilimia 3. 31 kwa kipande cha
Morogoro-Makutupora.
No comments :
Post a Comment