*Dola za Marekani milioni 100 kutumika katika ujenzi
Mkurugenzi wa Kukuza Uwekezaji kutoka Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Bw. John Mathew Mnali akizungumza jambo mbele ya waandishi wa Habari leo jijini Dar kuhusu masuala mbalimbali ya uwekezaji wa viwanda,ikiwemo na kuwapokea wageni wa uwekezaji wa viwanda kutoka nchini China na wenyeji wao kutoka kampuni ya Kiluwa Group Ltd.
MWENYEKITI wa Makampuni ya Kiluwa Group Ltd Mohammed Kiluwa (pichani kushoto) akifafanua jambo mbele ya Waandishi wa habari leo alipokwenda kuwatambulisha Wadau wake wa Uwekezaji katika masuala ya Viwanda kutoka nchini China,kwa kituo cha Uwekezaji nchini (TIC),na kueleza mikakati yao mbalimbali waliyonayo kuhusiana na uwekezaji wa viwanda nchini Tanzania,kulia ni Mkurugenzi wa Kukuza Uwekezaji kutoka Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Bw. John Mathew Mnali.
Wawekezaji wa Kampuni ya Yinengda New Material Techonology kutoka nchini China,wakiwa wameambatana na Mkurugenzi wao Mayi Hong wakisikiliza mambo mbalimbali yaliyokuwa yakizungumzwa kwenye mkutano huo,uliofanyika katika kituo cha Uwekezaji (TIC),jijini Dar
Mkurugenzi Mtendaji wa kituo cha Uwekezaji (TIC),Geofrey Mwambe akisalimia na Mkurugenzi wa kampuni ya Kiluwa Group,Naima Mohamed Kiluwa,walipokwenda kwenye ofisi za kituo hicho kuwatambulisha wadau wao wa uwekezaji katika mambo ya Uwekezaji wa Viwanda,anaeshuhudia pichani kati Mwenyekiti wa Kampuni ya Kiluwa Group,Mohamed Kiluwa (pichani kati) na kuwasilisha mikakati yao mbalimbali ya uwekezaji wa viwanda.
Mkurugenzi Mtendaji wa kituo cha Uwekezaji (TIC),Geofrey Mwambe akimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Yinengda New Material Techonology Mayi Hong alipokuwa akifafanua jambo kuhusiana na mambo ya uwekezaji wa viwanda hapa nchini Tanzania,maara aada kuzungumza na waandishi wa habara katika ofisi za kituo hicho .
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Yinengda New Material Techonology Mayi Hong akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa kituo cha Uwekezaji (TIC),Geofrey Mwambe walipowasili leo kwenda kutambulishwa na Mdau wake Mkubwa kwenye mambo ya Uwekezaji wa Viwanda,Mwenyekiti wa Kampuni ya Kiluwa Group,Mohamed Kiluwa (pichani kati) na kuwasilisha mikakati yao mbalimbali ya uwekezaji wa viwanda.
*Ahimiza Watanzania kuwa wazalendo kwa nchi yao

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii
MWENYEKITI
wa Makampuni ya Kiluwa Group Ltd Mohammed Kiluwa amesema katika
kuhakikisha anaunga mkono jitihada za Rais Dk.John Magufuli za ujenzi wa
Tanzania ya viwanda amefanikiwa kuwashawishi wawekezaji kutoka nchini
China kuja kujenga viwanda kuwekeza nchini.
Kiluwa
amesema kupitia ushawishi wake na kwa kushirikiana na Kituo cha
Uwekezaji Tanzania(TIC) wawekezaji hao kutoka China wamekubali kujenga
kiwanda cha kuongeza thamani ya bidhaa za ngozi, Kiwanda cha Saa pamoja
na Kiwanda cha Simu na kwamba awamu ya kwanza ya uwekezaji huo jumla ya
dola za Marekani milioni 100 zitatumika.
Akizungumza
leo jijini Dar es Salaam kuhusu ujio wa wawekezaji hao Kiluwa amesema
viwanda hivyo vitajengwa Mlandizi mkoani Pwani na wakati wowote kuanzia
sasa baada ya kukamilisha taratibu zote ikiwemo za vibali ujenzi wa
viwanda hivyo utaanza mara moja.Pia amesema mbali ya kujengwa kwa
viwanda hivyo wawakezaji hao wameonesha nia ya kujenga kiwanda cha
kubangua korosho mkoani
Mtwara
na kinachoendelea sasa ni mazungumzo ambayo yanakwenda vizuri na hakuna
kitakachoshindikana.”Wawekezaji hawa wameonesha nia kujenga kiwanda cha
korosho na walikuwa tayari kwenda mkoani Mtwara kuona mazingira.”
Kiluwa
amefafanua kwenye mazungumzo yake na wawekezaji hao aliwagusia kuhusu
zao la korosho nchini na hivyo wamekubali kujenga kiwanda cha
korosho.Amezungmzia umuhimu wa wananchi kuwa na uzalendo kwa nchi yao
katika kuhakikisha wanashiriki kikamilifu kwenye ujenzi wa uchumi wa
nchi na hasa kuelekea ujenzi waTanzania ya viwanda.
“Tuwe
wazalendo kwa nchi yetu kwa kuhakikisha tunaunga mkono juhudi za
Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais Dk.John Magufuli katika kujenga
Tanzania yenye uchumi imara kupitia viwanda.Ni jukumu letu Watanzania
kusimama imara kufanikisha dhamira ya Rais wetu mpendwa,”amesema Kiluwa
na kuongeza kwa kutambua malengo ya Rais ameamua kushiriki kwa vitendo
kuhamasisha wawekezaji kuja kuwekeza nchini.
“Kushawishi
wawekezaji ni kazi ngumu lakini naifanya kwa moyo wangu wote huku
nikitanguliza uzalendo kwa taifa langu.Nitoe rai kwa wanaohusika na
utoaji wa vibali kuhakikisha wanatoa kwa wakati ili wawekezaji ambao
wanakuja kuwekeza waanze shughuli za uwekezaji nchi kwetu,”amesema
Kiluwa na kuongeza kuwa anafurahishwa pia na ushirikiano uliopo kati
yake na TIC.
Kwa
upande wake Mkurugenzi wa Kukuza Uwekezaji kutoka TIC John Mnali
amesema moja ya mikakati yao ni kuendelea kuhamasisha wawekezaji kuja
kuwekeza nchini Tanzania ambako kuna mazingira mazuri ya uwekezaji.Pia
amefafanua pamoja na kuandaa mazingira mazuri ya uwekezaji nchini
wamekuwa wakisaidia kuhakikisha wawakezaji wanapata vibali vyote muhimu
vinavyotakiwa katika uwekezaji.”Moja ya jukumu letu ni kuwasaidia
wawekezaji waweze kupata vibali kwa haraka ili waendelee na uwekezaji.”
Wakati
huo huo Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Yinengda New Material
Techonology Mayi Hong ambaye amesema wamefurashiwa na mazingira mazuri
ya uwekezaji ya nchini Tanzania na kutokana na
mazingira mazuri yamewavutia kuwekeza kwa kujenga viwanda hivyo katika eneo la Mlandizi mkoani Pwani.
“Tutajenga
kiwanda cha kuongeza thamani ya ngozi na kisha kutengeneza bidhaa
zitokanazo na ngozi.Pia tutajenga kiwanda cha saa na kiwanda cha
simu.Tumetenga Dola za Marekani milioni 100 kwa ajili ya viwanda
hivyo.Pia katika mazungumzo yetu na Kiluwa tumejadiliana kuhusu ujenzi
wa kiwanda cha korosho na tunaamini tutajenga,”amesema Hong.
Wakiwa katika picha ya pamoja
No comments :
Post a Comment