………………
Kamanda wa polisi
mkoani Pwani, Wankyo Nyigesa, akionyesha kiasi cha bangi kati ya magunia
ya bangi yaliyokamatwa. Picha na Mwamvua Mwinyi
………………..
NA MWAMVUA MWINYI, PWANI
JESHI la polisi
mkoani Pwani, limewakamata watu wawili (wanaume) wanaodaiwa kusafirisha
bangi gunia 17 ndani ya gari lao lenye namba za usajili T. 819 CYQ aina
ya prado.
Kamanda wa polisi mkoani hapo (ACP), Wankyo Nyigesa alithibitisha kutokea kwa tukio hilo.
Alisema kwamba
,majina ya watuhumiwa hao yanahifadhiwa ambapo wamewakamata baada ya
kupokea taarifa fiche kutoka kwa wasamalia wema .
Alieleza, walipokea
taarifa hizo kuwa watu hao walikuwa wanasafirisha shehena hiyo ya
bangi,wakipitia barabara ya Bagamoyo kuelekea Dar es salaam.
Nyigesa alitoa onyo,
kwa wale wanaofanya biashara hiyo, wanaotumia na kusafirisha kuacha mara
moja kwani inasababisha athari kwa afya na kuharibu vijana ambao ndio
nguvu kazi ya Taifa.
“Kama nilivyotangulia kusema kwa siku za hivi karibuni, hakuna mhalifu ama wahalifu watakaofurukuta mkoani hapa, “
“Kila atakaebainika
atakutana na operesheni TINDUA TINDUA ya uhalifu, hivyo ni vyema
wakaacha uhalifu, kusafirisha magendo, bangi kutumia madawa ya kulevya
kwani lazima ukikamatwa upate joto ya jiwe “alieleza Nyigesa.
Kamanda huyo aliiomba
jamii, wawatume popote na wamwite kokote na wakati wowote yeye
ataitika, na wasisite kushirikiana na polisi kwa kutoa taarifa za
wahalifu na uhalifu unapopangwa ili kukomesha uhalifu mkoani humo.
No comments :
Post a Comment