Wednesday, October 31, 2018

TAKUKURU MKOANI ARUSHA YAOKOA ZAIDI YA MILIONI 11


Na Vero Ignatus, Arusha
Imeelezwa kuwa Taasisi ya kupambana na Rushwa mkoa wa Arusha imepokea jumla ya malalamiko 108 kwa njia mbalimbali ikiwa ni jitihada za kupambana na rushwa mkoani hapo.
Akitoa ripoti ya miezi mitatu ya kiutendaji  Naibu mkuu wa Takukuru mkoa wa  Arusha Frida Wikesi amesema taarifa hizo zimehusu halmashauri mbalimbali katika mkoa, idara ya ardhi, Nida, afya, kilimo, elimu, serikali za vijiji na mahakama
Amesema jumla ya majalada 23 ya uchunguzi yalifunguliwa na yanaendelea kuchunguzwa ambapo chunguzi hizo zipo katika hatua mbalimbali, haswa zilizo katika muelekeo wa makosa ya rushwa. 
Aidha amesema sheria ya kupambana na rushwa namba 11 ya mwaka 2007 inashauri, ushauri yakinifu kutolewa kwa watoa taarifa kwa malalamiko yanayoonekana kutokuangukia kwenye sheria hiyo. 
'' Malalamiko mengi yanayowasilishwa yanahusiana na rushwa, aidha kwa kipindi tajwa jumla ya makosa mapya mawili (02)yamefikishwa mahakamani '' alisema
Hata hivyo amesema kuwa ofisi ya takukuru mkoa wa Arusha wamefanya dhibiti moja la rushwa, na kuendesha zoezi la ufuatiliaji wa kuziba mianya ya rushwa. 
'' Hadi kufikia mwezi septemba 2018 jumla ya mashauri 18 yaliendelea kusikilizwa mahakamani ambayo yalikuwa katika hatua mbalimbali za mahakama"alisema Wikesi
Katika kipindi tajwa TAKUKURU iliweza kuokoa jumla ya fedha kiasi cha 11,345,000 ambazo zililipwa kwa watumishi waliokua wakishughulikia maonyesho ya 88 kanda ya kaskazini mwaka 2017(10,055,00)  fedha zilizokuwa za ujenzi wa mahabara sekondari ya Ilkiding'a Arumeru sh 1,290,000 ambazo zilirejeshwa serikalini.

No comments :

Post a Comment