WADAU WATAKIWA KUENDELEA KUFANYA TATHMINI YA ELIMU NCHINI
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR
–TAMISEMI), Selemani Jafo akifunga Mkutano wa pamoja wa Wadau wa Elimu
nchini uliofanyika kwa siku nne Jijini Dodoma. Mkutano huo ulijadili
kuhusu mafanikio na changamoto za sekta ya elimu.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu,
Sayansi na Teknolojia Dkt. Ave Maria Semakafu akitoa neno la Utangulizi
wakati wa ufungaji wa Mkutano wa pamoja wa Wadau wa Elimu nchini
uliofanyika kwa siku nne Jijini Dodoma. Mkutano huo ulijadili kuhusu
mafanikio na changamoto za sekta ya elimu.
Baadhi ya wadau wa elimu
walioshiriki katika Mkutano wa pamoja wa Wadau wa Elimu nchini
uliofanyika kwa siku nne Jijini Dodoma. Mkutano huo ulijadili kuhusu
mafanikio na changamoto za sekta ya elimu.
Waziri wa Nchi
OR – TAMISEMI akiwa katika picha ya pamoja na Wanafunzi walioshiriki
kama Wadau wa Elimu katika Mkutano wa pamoja wa Wadau wa Elimu nchini
uliofanyika kwa siku nne Jijini Dodoma. Mkutano huo ulijadili kuhusu
mafanikio na changamoto za sekta ya elimu.
Makamu Mwenyekiti
wa Mtandao wa Elimu Tanzania (TENMET), Lydia Wilberd akitoa salamu za
asasi hiyo kabla ya kufungwa kwa Mkutano wa pamoja wa Wadau wa Elimu
nchini uliofanyika kwa siku nne Jijini Dodoma. Mkutano huo ulijadili
kuhusu mafanikio na changamoto za sekta ya elimu.
Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO
Wadau wa Elimu
wametakiwa kuendelea kufanya tathmini ya elimu kwa kujadili mafanikio na
changamoto za sekta hiyo ili kuboresha na kukuza elimu nchini.
Hayo
yamebainishwa jana jijini Dodoma na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais –
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR – TAMISEMI), Selemani Jafo
alipokuwa akifunga Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Wadau wa Elimu.
Waziri Jafo
amesema kuwa nchi nyingi ambazo hazina rasilimali za madini wala vivutio
vya utalii zinaendelea kuwekeza katika rasilimali elimu ambapo baadae
nchi hizo huwa tajiri na kutoa misaada kwa nchi masikini.
“Taifa
linalowekeza vizuri katika sekta ya elimu ndilo Taifa lenye nafasi kubwa
ya kukomboa wananchi wake na taifa kiujumla hivyo kutathmini juu ya
elimu inayotolewa nchini kwetu ni jambo la muhimu sana”, alisema Jafo.
Waziri Jafo
amewasisitiza wadau wa elimu walioshiriki katika mafunzo hayo kutekeleza
maazimio yote yaliyoazimiwa kwenye kikao hicho ili kuendelea kutoa
matokeo chanya katika sekta hiyo.
Vile vile ametoa
rai kwa wadau wa elimu kuendelea kutoa michango yao ya hali na mali
katika kuinyanyua sekta ya elimu nchini ili kwa pamoja taifa la Tanzania
liweze kujinasua katika umasikini kupitia elimu.
Aidha, amewataka
wadau wa elimu kuwa huru katika kutoa mawazo yao bila kuogopa na
kuwahakikishia kuwa milango ya ofisi hiyo iko wazi kukubali changamoto
mbalimbali zinazopelekwa na inaendelea kuzitatua.
Kwa upande
wake Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt.
Ave Maria Semakafu amesema kuwa kwa pamoja mkutano huo umejadili juu ya
uboreshaji wa elimu nchini hasa juu ya suala la uwazi katika mipango na
utekelezaji wa bajeti za elimu.
“Ili kuboresha
sekta ya elimu nchini uwazi ni jambo la msingi hivyo tunawaomba wenzetu
wa mashirika na taasisi tunaosaidiana katika sekta hii wajitahidi kuweka
bajeti zao wazi kama Serikali inavyofanya ili kuboresha zaidi sekta
hii”, amesema Dkt. Ave Maria.
Mkutano huo
umeshirikisha wadau mbalimbali wakiwemo Wakurugenzi, Maafisa Elimu wa
Mikoa na Wilaya pamoja na Taasisi zisizo za kiserikali.
No comments :
Post a Comment