Sunday, September 30, 2018

PRINCE WILLIAM AIPAISHA SAME KIMATAIFA, NI BAADA YA KULALA KWA SIKU MBILI KWENYE HIFADHI YA TAIFA MKOMAZI ILIYOKO WILAYANI HUMO

 Mjukuu wa Malkia wa Uingereza, Prince William (wapili kushoto), Mkuu wa Wilaya ya Same, Mhe. Rosemary Senyamule (watatu kushoto), Mwenyekiti wa Bodi ya Uhifadhi wa Faru, Dkt. Bernad Mchomvu (wakwanza kushoto) na Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA, Dkt.Allan Kijazi, wakifurahia jambo kwenye hema maalum lililojengwa kama makazi ya muda ya Mjukuu huyo wa Malkia kwenye hifadhi ya taifa Mkoamazi Wilayani Same Mkoa wa Kilimanjaro.
NA K-VIS BLOG, MKOMAZI SAME 
MJUKUU wa Malkia wa Uingereza Prince William, ametumia siku mbili kati ya tatu alizotembelea nchini Tanzania kupumzika Wilayani Same Mkoani Kilimanjaro. Prince William ambaye aliwasili nchini Septemba 23 alilala Dar es Salaam kwa siku hiyo moja, na kisha baada ya kumaliza ziara yake jijini Dar es Salaam, kwa kukutana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli, na kisha kutembeela bandari ya Dar es Salaam kabla ya kuelekea Wizara ya Maliasili na Utalii kwenye ofisi zake ndogo za Dar es Salaam, Prince William aliamua kufanya mapunziko yake binafsi eneo la Mkoamazi, Wilayani Same.
Siku hizo mbili alizotumia Mjukuuwa Mfalme kupumzika kwenye eneo la hifadhi ya Mkomazi inaelezwa kuhamasisha na kuitangaza hifadhi hiyo kimataifa kuwa kati ya hifadhi zenye mvuto mkubwa Afrika Ziara ya Prince William barani Afrika, ilianzia nchini Namibia, Tanzania na kisha Kenya, ililenga kuangalia juhudi za serikali za Afrika katika kukabiliana na ujangili na biashara ya haramu ya wanayamapori, ili hatimaye atoe ripoti kwenye mkutano mkubwa wa kidunia utakaofanyika baadaye jijini Lon don Uingereza kujadili namna ya kuzuia biashara haramu ya wanyamapori duniani. Aidha akiwa wilayani Same, Prince William alipokea taarifa ya uongozi wa Wilaya hiyo katika mapambano ya kuzuia biashara haramu ya wanyama pori na hivyo kuonyesha dhamira ya kusaidia mapambano dhidi ya ujangili. Pia aliahidi kushiriki ukuzaji wa utalii kwa mipango ya Wilaya na TANAPA.  Mjukuu huyo wa Mfalme aliwaachia ujumbe viongozi wa Wilaya na Watanzania kwa ujumla ikiwemo TANAPA, kuhakikisha utalii unahusisha wananchi wanaozunguka hifadhi. kwa kuzingatia utekelezaji wa mipango mikubwa ya kuiboresha inayoendelea. Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Same, Mhe. Rosemary Senyamule aeleza ukamilishaji wa mpango mkakati ya kukuza utalii Wilayani utakao unganisha utalii wa hifadhi ya taifa ya Mkomazi, Mlima Shengena, msitu wa Chome pamoja na utalii wa asili/ utamaduni. Pia alimueleza fursa za uwekezaji zilizopo wilayani humo ikiwa ni pamoja na kumkaribisha kuwekeza. Naye Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA Dr. Allan Kijazi amueleza juu ya hifadhi za TANAPA na uhitaji wa kuongeza nguvu ya kupambana na ujangili na kumualika aje tena nchini kutembelea mbuga nyingine. 
 Prince William akitambulishwa kwa Mkuu wa Wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro baada ya kutua kwenye hifadhi ya taifa ya Mkomazi wilayani humo.

Prince William akisali miana na Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA, Dkt. Allan Kijazi

No comments :

Post a Comment