Saturday, September 29, 2018

CBA YATOA MSAADA WA MILIONI 4 SHULE YA SINGISI


 
Mkuu wa Idara ya wateja ,masoko na mawasiliano benki ya CBA,Julius Konyani  Akikabidhi hundi ya shilingi milioni 4 kwa Mkuu wa Shule ya Msingi Singisi ,Safira Ndelwa.Benki hiyo imetoa msaada huo kwa
ajili ya mabati na ukarabati wa madarasa.Picha na Pamela Mollel,Arusha 
Mkuu wa Idara ya wateja ,masoko na mawasiliano benki ya CBA,Julius Konyani  Akikabidhi hundi ya shilingi milioni 4 kwa Mkuu wa Shule ya Msingi Singisi ,Safira Ndelwa.Benki hiyo imetoa msaada huo kwa ajili ya mabati na ukarabati wa madarasa 

Mkuu wa Idara ya wateja ,masoko na mawasiliano benki ya CBA,Julius Konyani akizungumza
katika hafla ya kukabidhi hundi ya milioni 4 kwa ajili ya kusaidia shule ya
msingi Singisi.
 Mkuu wa Idara ya wateja ,masoko na mawasiliano benki ya CBA,Julius Konyani  akikabidhi hundi kwa mwanafunzi wa shule ya msingi Singisi
 Mkuu wa Idara ya wateja ,masoko na mawasiliano benki ya CBA,Julius Konyani  akipokea zawadi kutoka wanafunzi wa shule ya msingi Singisi.
 Picha ya pamoja
CBA YATOA MSAADA WA MILIONI 4 SHULE
YA SINGISI
Na Pamela Mollel,Arusha.
Benki ya  CBA imetoa msaada wa shilingi milioni 4 kwa shule ya msingi Singisi kwa ajili ya mabati pamoja na ukarabati wa shule hiyo ili kusaidia kutatua changamoto ya uhaba wa madarasa na uchakavu wa majengo.
Mkuu wa Idara ya wateja ,masoko na mawasiliano,Julius Konyani  alisema kuwa wameamua kutoa msaada huo ili kusaidia  watoto wa kitanzania waweze kupata elimu bora ambayo itawasaidia kujikwamua kiuchumi na kuondokana na umasikini.
 
Julius alisema kuwa benki hiyo imeamua kurudisha sehemu ya faida kwa wananchi kwa kutoa fedha hizo licha ya msaada huo wamekua wakisaidia chumba cha watoto njiti kwa kutoa
vifaa vya kitaalamu ili kuokoa maisha ya watoto.
 
Mkuu wa Shule hiyo Safira Ndelwa    ameshukuru msaada huo ambapo amesema kuwa msaada huo utawasaidia kumalizia ujenzi wa uzio wa shule hiyo pamoja na kukarabati majengo ya shule hiyo ambayo ni chakavu.
 
Hata hivyo ameiomba benki hiyo iweze kuwasaidia kuwajengea vyumba vya madarasa kwani shule hiyo inakabiliwa na uhaba wa madarasa hali inayosababisha msongamano darasani
inayowalazimu kuingia darasani kwa awamu huku walimu wakifundisha kwa zamu.
 
“Tunaomba benki ya CBA isituache iendelee kutusaidia katika maeneo mengine ambayo kuna
changamoto ili wanafunzi waweze kusoma katika hali bora” Alisema
 
Diwani wa Kata ya Seela Singisi Penzila Palangyo amesema kuwa ushiriki wa sekta binafsi
katika maendeleo ya elimu ni muhimu ili kuhakikisha kuwa sekta ya elimu
inasonga mbele na kusaidia maisha ya watu wengi

No comments :

Post a Comment