Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akioneshwa mipaka ya
Pori la Akiba Kijereshi na Meneja wa pori hilo, Dianna Chambi
alipotembelea pori hilo jana kwa ajili ya kukagua shughuli za uhifadhi
katika wilaya ya Busega mkoani Simiyu. Alitoa siku 45 kwa wananchi wote
waliovamia kingo/bafa za hifadhi hiyo kuondoka kwa hiari yao. Kulia ni
Mkuu wa Kanda wa Kikosi Dhidi ya Ujangili (KDU) Kanda ya Serengeti,
Johnson Msella.
Na Hamza Temba-Simiyu
…………………………………………………
*Atoa miezi mitatu kwa Muwekezaji kurudisha Serikalini hati miliki ya kipande cha ardhi kilichopo ndani ya Pori hilo
Waziri wa Maliasili
na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla amewapa siku 45 wananchi wanaoishi
kinyume cha Sheria ndani ya kinga (bufer zone) za Pori la Akiba
Kijereshi kuondoka kwa hiari yao wenyewe kabla ya kuanza operesheni ya
kuwaondoa kwa nguvu.
Ametoa agizo hilo
jana alipotembelea pori hilo katika wilaya ya Busega mkoani Simiyu ikiwa
ni muendelezo wa ziara zake mikoani kwa ajili ya kukagua shughuli za
uhifadhi na kutatua changamoto zake.
Baada ya kushuhudia
makazi na shughuli nyingine za kibinadam ndani ya pori hilo, Dk.
Kigwangalla aliamua kutoa agizo hilo na kusema kuwa sheria za uhifadhi
wa wanyamapori haziruhusu vitendo hivyo ndani ya maeneo yaliyohifadhiwa
kisheria pamoja na kingo zake (buffer zone) ambazo ni mita 500 kutoka
kwenye mpaka halisi wa eneo la hifadhi.
“Mpaka itakapofika
tarehe 31 mwezi ujao (Septemba) wananchi wote hawa wawe wameshaondoka
eneo hili kwa hiari yao wenyewe, muwatangazie na mpime eneo hili vizuri
muweke alama ili wajue ni wapi wanatakiwa kuondoka.
“Na ikifika tarehe 1
Septemba kama kuna watakaokuwa wamekaidi agizo hili, basi mfanye
oparesheni maalum muwaondoe na msafishe kila kitu, ni lazima ifike
mahali kila mmoja aheshimu sheria za nchi” alisema Dk. Kigwangalla
kuuagiza uongozi wa pori hilo.
Wakati huo huo,
Waziri Kigwangalla ametoa miezi mitatu kwa muwekezaji wa hoteli ya
kitalii ya Kijereshi Tented Camp kurudisha kwa Kamishna wa Ardhi hati
miliki ya kipande cha ardhi chenye ukubwa wa hecta 464 kilichopo ndani
ya pori hilo kwakuwa ni batili.
Aimesema pori hilo
lilianzishwa mwaka 1994 wakati muwekezaji huyo anadai kumilikishwa eneo
hilo mwaka 1995 jambo ambalo haliwezekani mtu binafsi kupewa hati ya
kumiliki eneo lililopo ndani ya eneo jingine tena hifadhi.
Aidha, amemtaka pia
muwekezaji huyo kuheshimu sheria na taratibu za uwekezaji katika eneo
hilo ikiwemo kulipa ada na tozo mbalimbali.
Pori la Akiba
Kijereshi lenye ukubwa wa kilomita za mraba 65.72 linasimamiwa na
Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania TAWA na lilipandishwa hadhi
kuwa Pori la Akiba mwaka 1994 kwa Tangazo la Serikali Na. 215 la terehe
10 Juni, 1994 na hiyo ni kutokana na umuhimu wake kiuchumi na
kiikolojia hususan katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akitoa maelekezo kwa
Meneja wa Pori la Akiba Kijereshi, Dianna Chambi (wa pili) kuhusu
wananchi waliovamia hifadhi hiyo alipotembelea pori hilo jana kwa ajili
ya kukagua shughuli za uhifadhi katika wilaya ya Busega mkoani Simiyu.
Waziri wa Maliasili na Utalii,
Dk. Hamisi Kigwangalla akikagua eneo la hoteli ya kitalii ya Kijereshi
Tented Camp iliyopo ndani ya Pori la Akiba Kijereshi alipotembelea pori
hilo jana kwa ajili ya kukagua shughuli za uhifadhi katika wilaya ya
Busega mkoani Simiyu, ametoa miezi mitatu kwa mmiliki wa hoteli hiyo
kurudisha hati miliki ya kiwanja chenye hekta 464 kilichopo ndani ya
pori ya pori hilo kwa kamishna wa ardhi kwakuwa ni batili na aendelee
kutoa huduma kwa kuzingatia sheria na taraibu za uwekezaji.
Waziri wa Maliasili na Utalii,
Dk. Hamisi Kigwangalla akifungua koki ya maji katika eneo la hoteli ya
kitalii ya Kijereshi Tented Camp iliyopo ndani ya Pori la Akiba
Kijereshi alipotembelea pori hilo jana kwa ajili ya kukagua shughuli za
uhifadhi katika wilaya ya Busega mkoani Simiyu, ametoa miezi mitatu kwa
mmiliki wa hoteli hiyo kurudisha hati miliki ya kiwanja chenye hekta 464
kilichopo ndani ya pori hilo kwa kamishna wa ardhi kwakuwa ni batili na
aendelee kutoa huduma kwa kuzingatia sheria na taraibu za uwekezaji.
Waziri wa Maliasili na Utalii,
Dk. Hamisi Kigwangalla akizungumza na wananchi wa kijiji cha Logolambogo
katika wilaya ya Itilima mkoani Simiyu alipolitembelea Pori la Akiba
Maswa jana kwa ajili ya kukagua shughuli za uhifadhi na kutatua
changamoto zake.
Waziri wa Maliasili na Utalii,
Dk. Hamisi Kigwangalla akizungumza na wananchi wa kijiji cha Logolambogo
katika wilaya ya Itilima mkoani Simiyu alipolitembelea Pori la Akiba
Maswa jana kwa ajili ya kukagua shughuli za uhifadhi na kutatua
changamoto zake.
Waziri wa Maliasili na Utalii,
Dk. Hamisi Kigwangalla akizungumza na wananchi wa kijiji cha Logolambogo
katika wilaya ya Itilima mkoani Simiyu alipolitembelea Pori la Akiba
Maswa jana kwa ajili ya kukagua shughuli za uhifadhi na kutatua
changamoto zake.
Waziri wa Maliasili na Utalii,
Dk. Hamisi Kigwangalla akizungumza na wananchi wa kijiji cha Logolambogo
katika wilaya ya Itilima mkoani Simiyu alipolitembelea Pori la Akiba
Maswa jana kwa ajili ya kukagua shughuli za uhifadhi na kutatua
changamoto zake.
Waziri wa Maliasili na Utalii,
Dk. Hamisi Kigwangalla akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony
Mtaka alipowasili mkoani humo jana kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku
moja ya kukagua shughuli za uhifadhi na kutatua changamoto zake.
Waziri wa Maliasili na Utalii,
Dk. Hamisi Kigwangalla akikagua moja ya eneo la kingo/bafa la Pori la
Akiba Maswa ambalo limevamiwa na wananchi kwa ajili ya shughuli kilimo
alipolitembelea pori hilo jana kwa ajili ya kukagua shughuli za uhifadhi
katika wilaya ya Itilima mkoani Simiyu. Kulia kwake ni Mbunge wa
Itilima, Njaru Silanga na Meneja wa Pori hilo, Lusajo Masinde.
No comments :
Post a Comment