Katibu
Mtendaji Bodi ya Filamu Tanzania Joyce Fissoo akionyesha moja ya leseni inayotolewa
na Bodi ya Filamu Tanzania kwa wadau wa sekta ya filamu Mkoa wa Songwe (hawapo
pichani) zinazotolewa na Ofisi yake kwa waandaaji wa kazi za filamu nchini katika madaraja mbalimbali kulingana na
uzoefu, katika warsha ya mafunzo ya kuwajengea uwezo wadau hao iliyofanyika leo
Mjini Vwawa,Wilayani Mbozi Mkoani hapo .
Naibu
Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bw.Nicholaus William (katikati)
akiwataka wadau wa sekta ya Filamu Mkoani Songwe (hawapo pichani) kutumia fursa
za kiutalii na mazingira mazuri ya Mkoa huo kuandaa kazi za filamu alipokuwa
akifungua warsha ya siku mbili ya mafunzo ya kuwajengea uwezo wadau hao
iliyofanyika Mjini Vwawa Wilayani Mbozi,kutoka kushoto ni Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Tanzania
Joyce Fissoo na kulia ni Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Songwe Bw.Juma Mhina.
Mmoja
wa watoa Mada Dkt.Vicenisia Shule akitoa Mada ya Uandaaji wa Miswada ya Filamu
kwa wadau wa sekta ya filamu Mkoani Songwe (hawapo pichani) katika warsha ya
siku mbili iliyoandaliwa na Bodi ya filamu Tanzania iliyofanyika Mjini
Vwawa,Wilayani Mbozi kwa lengo la
kuwajengea uwezo wasanii hao.
Katibu
Mtendaji Bodi ya Filamu Tanzania Joyce Fissoo (kushoto) akisikiliza swali la
mmoja wa wadau wa sekta ya filamu mkoani Songwe Bw.Barick Mbogella aliyehudhuria
warsha ya mafunzo ya kuwajengea uwezo wadau wa sekta ya felamu mkoani hapo, iliyoandaliwa
na Bodi ya Filamu Tanzania na kufanyika leo katika Mji wa Vwawa,Wilayani Mbozi.
Katibu
Umoja wa Wanatasnia wa Filamu Mkoa wa Songwe Bw.Tegemea Hasunga akichangia mada
ya uandaaji wa Miswada ya kazi za filamu katika warsha ya mafunzo ya kuwajengea
uwezo wadau wa sekta ya filamu Mkoani Songwe iliyoandaliwa na Bodi ya Filamu
Tanzania na kufanyika leo Mjini Vwawa,Wilayani Mbozi.
Baadhi
ya wadau wa sekta ya Filamu Mkoa wa Songwe wakiwa katika picha ya pamoja na
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bw.Nicholaus
William aliyeketi meza kuu (wapili kutoka kulia) mara baada ya ufunguzi wa
warsha ya mafunzo ya kuwajengea uwezo wadau wa sekta ya filamu wa mkoa
huo,yaliyoandaliwa na Bodi ya Filamu Tanzania na kufanyika Mjini Vwawa,Wilayani
Mbozi,A kutoka kushoto wa pili Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Tanzania Bibi.
Joyce Fissoo na kutoka kulia wapili ni Kaimu Afisa Tawala Mkoa wa Songwe Bw.
Juma Mhina na wa kwanza kulia ni Katibu Mkuu wa Shirikisho la Filamu Tanzania
Bw.Mathew Nicolaus.
NA
ANITHA JONAS – VWAWA,MBOZI
WADAU
wa sekta ya Filamu Mkoa wa Songwe waelezwa kutumia fursa zilizoko Mkoani hapo ikiwemo
uwepo wa maeneo mazuri ya asili naya kiutamaduni kwa ajili ya kuandaa filamu za
Kiutamaduni.
Kauli
hiyo imetolewa leo Wilayani Mbozi, Mjini Vwawa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari
Utamaduni Sanaa na Michezo Bw.Nicholaus William alipokuwa akifungua warsha ya siku
mbili ya kuwajengea uwezo wadau wa sekta ya filamu mkoanI Songwe.
“Mkoa
wa Songwe umebarikiwa kwa kuwa na fursa nyingi ikiwemo uwepo wa Kimondo ambacho
ni kivutio kikubwa cha utalii pamoja na mandhari nzuri ya mkoa huu ambayo
imekuwa ni kivutio kikubwa kwa wapiga picha wa kimataifa wanaokuja kupiga picha
katika mkoa huu kwa ajili ya kuandaa Makala mbalimbali,”alisema Bw.William.
Akiendelea
kuzungumza katika warsha hiyo Naibu Katibu Mkuu huyo alisisitiza kuwa ni lazma
kazi za filamu kuandaliwa kwa uweledi ili sekta ya filamu nchini iweze kushindana vyema na soko la filamu Afrika na
Duniani kwa ujumla na kwa kuzingatia hilo filamu zenu zitaweza pia kushinda
tuzo za kimataifa.
Kwa
upande wa Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu
Tanzania Bibi. Joyce Fissoo alitoa elimu
kwa wadau hao wa filamu kwa kuwaeleza majukumu ya bodi ya filamu pamoja na
kuwaeleza kuwa bodi ya filamu imekuwa ikitoa leseni na vitambulisho kwa ajili
ya utambulisho wa wadau wanaojihusiha na kazi za filamu na hifadhi kanzi data ya wadau
wa filamu nchini.
“Suala
la ukaguzi wa kazi za filamu kwa mikoani kuanzia ngazi ya miswada inakaguliwa
katika Halmashauri kupitia bodi zilizoundwa kupitia Afisa Utamaduni pamoja na wajumbe mbalimbali hivyo msanii wa
mkoani mswada wa kazi yake ya filamu na filamu yake inakaguliwa nao na halazimiki
kuja mpaka Dar es Salaam,”alisema Bibi Fissoo.
Pamoja
na hayo Katibu Mtendaji huyo alieleza kuwa warsha hiyo itatoa mafunzo ya aina
mbalimbali ikiwemo somo la Uandaaji wa Miswada ya Filamu,Somo la kijitangaza
(Branding),Matumizi ya Mitandao na Matumizi ya lugha ya Kiswahili na masomo
mengine yanayosaidia sekta ya filamu.
Mbali
na hayo nae mmoja wa wasilishaji mada ambaye ni Mjumbe wa Bodi ya Filamu nchini
Dkt. Vicenisia Shule aliwaeleza wadau hao wa filamu kuwa serikali inandaa Sera
ya Filamu ambayo itasaidia kutoa mwongozo wa kuisimamia vyema sekta ya filamu
kwa kuzingatia sheria inayosimamia sekta ya filamu nchini kwa sasa.
Hata
hivyo warsha hiyo inatarajiwa kumalizika Julai,20 mwaka huu ambapo sherehe za
ufungaji zitafanywa na Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo
Mhe.Juliana Shonza.
No comments :
Post a Comment