Kampuni za MultiChoice Tanzania na
UBER zimetangaza ushirikiano maalum ambapo kwa sasa madereva wa UBER
wanaweza kuwa mawakala wa DStv na na pia wateja wa DStv kupata punguzo
maalum kwa safari zao kutumia UBER.
Katika ushirikiano huo,
medereva wote wa UBER wataweza kupata seti ya DStv kwa shilingi 69,000
tu pamoja na kifurushi cha mwezi mmoja bure.
Kwa wateja wa DStv ambao wanapakua
App ya UBER kwa mara ya kwanza watapata punguzo la shilingi 6,200 kwa
safari yao ya kwanza na UBER
Afisa Mauzo wa MultiChoice
Tanzania Gloria Anderson (katikati) akiongea wakati wa hafla ya
kutangaza ushirikiano kati ya DStv na UBER utakaowawezesha wateja wa
DStv kupata punguzo maalum wanapotumia usafiri wa UBER na pia madereva
na wafanyakazi wa UBER kupata ofa maalum wananuapo DStv.
Mkuu wa Mawasiliano wa MultiChoice
TanzaniaJohnson Mshana (Kulia) akiongea wakati wa hafla ya kutangaza
ushirikiano kati ya DStv na UBER utakaowawezesha wateja wa DStv kupata
punguzo maalum wanapotumia usafiri wa UBER na pia madereva na
wafanyakazi wa UBER kupata ofa maalum wananuapo DStv. Kutoka kushoto ni
Afisa Masoko wa MultiChoice Gloria Anderson, Balozi maalum wa DStv Nancy
Sumari na Afisa muandamizi wa UBER Davis Evans
Balozi maalum wa DStv Nancy Sumari
akizungumza katika hafla hiyo iliyofanyika Mlimani City jijini Dar es
Salaam. Kulia ni Afisa Muandamizi wa UBER Davis Evans
Afisa muandamizi wa UBER Davis
Evans akitoa maelezo kuhusu ushirikiano kati yao na DStv. Katikati ni
balozi maalum wa DStv Nancy Sumari na kushoto ni Afisa Mauzo wa
MultiChoice Tanzania Gloria Anderson.
No comments :
Post a Comment