Kaimu mkurugenzi mtendaji wa Tume
ya kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS ),Jumanne Issango ,akifungua
mkutano ulioandaliwa na Tume hiyo kwa lengo la kupitia mipango kazi ya
utekelezaji wa afua za ukimwi kwa asasi mwamvuli, mitandao ya watu
wanaoishi na virusi/ Ukimwi pamoja na sekta binafsi, Mjini Kibaha Mkoani
Pwani
Baadhi ya washiriki wakisikiliza
jambo kwa makini wakati wa mkutano ulioandaliwa na Tume ya kudhibiti
Ukimwi Tanzania (TACAIDS) kwa lengo la kupitia mipango kazi ya
utekelezaji wa afua za ukimwi kwa asasi mwamvuli, mitandao ya watu
wanaoishi na virusi/ Ukimwi pamoja na sekta binafsi, Mjini Kibaha Mkoani
Pwani.
Picha ya pamoja ya washiriki
waliohudhuria mkutano ulioandaliwa na Tume ya kudhibiti Ukimwi Tanzania
(TACAIDS) kwa lengo la kupitia mipango kazi ya utekelezaji wa afua za
ukimwi kwa asasi mwamvuli, mitandao ya watu wanaoishi na virusi/ Ukimwi
pamoja na sekta binafsi, Mjini Kibaha Mkoani Pwani.
Picha na Mwamvua Mwiny
………
Na Mwamvua Mwinyi, Pwani
TUME ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania
(TACAIDS), imeitaka jamii kukataa maambukizi mapya ya Ukimwi pamoja
na taasisi mwamvuli kuhakikisha zinapanga mipango mkakati ili kuondokana
na maambukizi hayo ifikapo 2030.
Aidha imewaasa wanaoishi na Virusi
Vya Ukimwi, kutumia dawa za kufubaza virusi hivyo
(ARVs) kikamilifu,
badala ya kukatisha dozi na kukimbilia kwa waganga wa kienyeji, kwani
kwa kufanya hivyo kusababisha madhara na vifo dhidi yao.
Hayo yalisemwa na kaimu mkurugenzi
mtendaji wa TACAIDS ,Jumanne Issango ,wakati akifungua mkutano
ulioandaliwa na Tume hiyo kwa lengo la kupitia mipango kazi ya
utekelezaji wa afua za ukimwi kwa asasi mwamvuli, mitandao ya watu
wanaoishi na virusi/ Ukimwi pamoja na sekta binafsi, Mjini Kibaha Mkoani
Pwani.
Issango alibainisha, malengo ya
kitaifa ni kuwa na 90 tatu, ambapo asimilia 90 ya kwanza ni ya watu
wanaoishi na virusi vya ukimwi nchini ambao bado hawajajitambua afya zao
kuhakikisha wawe wamepima ifikapo mwaka 2020.
Pia ,wanaoishi na virusi vya
ukimwi ifikapo 2020 wawe wameingia katika kutumia dawa za kufubaza VVU
na ifikapo mwaka huo asilimia 90 ya ambao wanatumia dawa hizo wawe na
virusi vilivyokuwa tayari vimefubaa.
Kwa mujibu wa kaimu huyo, malengo
hayo ni makubwa na ndio maana wameitana ili kila mmoja katika asasi yake
aone namna watakavyoshirikiana kutimiza 000 na ifikapo 2030
kuondoa maambukizi mapya ya UKIMWI,Unyanyapaa na Vifo.
Alisema waliogundulika na
maambukizi ya VVU ni vyema wakafuata masharti ya daktari na kutumia dawa
bila kufanya mzaha wala ajizi.
Issango alieleza ,wapo baadhi ya
wenye virusi hivyo, ambao hawakuona umuhimu wa kufuata masharti
wanayopewa jambo limewasababishia kupoteza maisha yao.
“Sio rahisi kumaliza ukimwi kabisa
ifikapo 2030 lakini kwa kufanya kazi kwa makundi yote ,kupima afya zetu
bila uoga, kuacha kuambukizana kwa makusudi, kutumia dawa kikamilifu,
kuacha ngono zembe ,kwa hakika tutafikia malengo hayo”alisisitiza
Issango.
Alieleza , malengo ya kitaifa ni
kufikia watu katika upimaji na kuwaingiza katika dawa na kuhakikisha
kunakuwa na ufuasi mzuri wa matumizi mazuri ya dawa hizo.
Nae Mwenyekiti wa chama cha walimu
wanaoishi na VVU/UKIMWI (TAPOTI –Taifa) Mwl.Helen Masao, alisema walimu
wengi ni waoga wa kupima afya zao.Alisema wapo ambao wameshapima lakini
wanapenda kuhahama kwenye CTC walizoanza na kuhamia kwenye maeneo ,ama
wilaya na mikoa mingine kwa lengo la kujificha wasijulikane.
Masao alisema hali hiyo
inasababisha baadhi ya walimu hao kuambukiza wengine ama wanafunzi ambao
wanakubaliana kwenye mahusiano ya kimapenzi.
Aliishukuru CWT kwa ushirikiano wao na kuitaka kuendelea kutambua na kujali walimu walio na maambukizi ya virusi vya Ukimwi .
Kwa upande wake, mkurugenzi
mtendaji mtandao wa wanawake wanaoishi na VVU Tanzania ,Joan Chamungu
alieleza asasi yao ikabiliwa na changamoto ya raslimali fedha, watu
kuuzoea Ukimwi kuuona ni ugonjwa wa kawaida na Unyanyapaa has Vijijini.
Mwakilishi kutoka Restless
Development Youth Organization ,Chuo kikuu cha ardhi Dar es salaam ,Bi
Salome Jacob alisema baadhi ya vijana wanapata maambukizi mapya ya
Ukimwi kutokana na tamaa na wengine kushawishika kufanya mapenzi na
walimu ili kufaulishwa katika masomo yao.
“Wanafunzi wa kike vyuoni wapo
wanaoshinikizwa kufanya tendo la ndoa na walimu ambao wengine tayari
wameambukizwa, hivyo kusababisha mlolongo mkubwa wa maambuki mpaya kwa
wanachuo”alisema Salome.
Salome alisema asasi yao
unahahakisha kuna maendeleo chanya kwa vijana hasa vyuoni na kutoa elimu
dhidhi ya kuepuka ugonjwa wa Ukimwi ili kufikia malengo ya kitaifa ya
kupambana na ugonjwa huo.
Taasisi mwamvuli zilizoshiriki
katika mkutano huo ni Baraza la Taifa la NG’O (NACONGO), Chama cha
waajiri Tanzania (ATE), Chama cha walimu wanaoishi na VVU/UKIMWI
(TAPOTI),TUCTA, Tanzania private sectors foundation (TPSF),Restless na
Baraza la hiari la maendeleo ya jamii (TACOSODE).
No comments :
Post a Comment