Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Waziri wa
Mambo ya Nje wa Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani Mhe. Heiko Maas,
Ikulu jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya
pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje wa Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani
Mhe. Heiko Maas wengine pichani kulia ni Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Augustine Mahiga (kulia) na
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Zanzibar Mhe. Issa Gavu, Ikulu jijini Dar
es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiagana na Waziri wa
Mambo ya Nje wa Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani Mhe. Heiko Maas mara
baada ya mazungumzo Ikulu jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Waziri wa
Mambo ya Nje wa Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani Mhe. Heiko Maas,
Ikulu jijini Dar es Salaam.
Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais
……………
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo amekutana na
kuzungumza na Waziri wa Mambo ya Nje wa Shirikisho la Jamhuri ya
Ujerumani Mhe. Heiko Maas.
Makamu wa Rais amesema kwa pamoja
wamekubaliana kusaidiana katika kuleta utaalamu na teknolojia kwenye
viwanda vyetu hapa Tanzania haswa kwenye maeneo ya Kilimo, Uchimbaji
Madini na Viwanda vya Madawa.
Makamu wa Rais asema Tanzania na
Ujerumani wana Historia ya miaka mingi hivyo wamekubalina pia kujenga
uwezo kwenye mambo ya uhifadhi ili kuvumbua mambo zaidi ambayo yapo
Tanzania ili kukuza Utalii wa kuonyesha mambo ya Tanzania na Historia
yake.
Makamu wa Rais amewashukuru kwa
msaada wa masuala ya Afya haswa Afya ya Mama na Mtoto pamoja na
uendelezaji wa shughuli za Utalii.
Makamu wa Rais aliwaomba
tusaidiane katika kuzalisha umeme zaidi hapa Tanzania na kuwataka pia
kuleta wawekezaji Zaidi Tanzania na wamekubalina hayo.
Kwa Upande wake Waziri wa Mambo ya
Nje wa Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani Mhe. Heiko Maas alisema
amefurahi kutembelea Tanzania na ameisifia ni nchi nzuri sana na kuahidi
kuendelea kwa Ushirikiano pamoja na kuendelea kusaidia katika masuala
mbali mbali ya kuleta maendeleo.
Katika Mkutano huo , Waziri wa
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Augustine Mahiga
pamoja na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza
la Mapinduzi Mhe. Issa Gavu walihudhuria.
No comments :
Post a Comment