Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki imepokea fursa za ufadhili wa masomo ya
muda mrefu katika sekta ya miundombinu chini ya program iitwayo “Global Infrasructure Development Scholarship Program (GIDSP) kutoka Jamhuri ya Korea.
Mafunzo haya ambayo ni kwa ajili
ya Watumishi wa Umma yatafanyika katika Chuo Kikuu cha Seoul (UOS)
nchini Korea kuanzia mwezi Agosti 2018 hadi Desemba 2019.
Waombaji wa mafunzo haya
wanatakiwa kutuma maombi yao moja kwa moja kwenye Chuo Kikuu cha Seoul
(UOS). Maelezo ya ziada kuhusu mafunzo haya na namna ya kutuma maombi
yanapatikana kupitia tovuti ya http://isus.uos.ac.kr au maombi yatumwe kwa barua pepe ifuatayo: mipd@uos.ac.kr. Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 18 Mei, 2018.
Mafunzo haya yanaratibiwa na Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.
No comments :
Post a Comment