Kaimu
Mkuu wa Ofisi za Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu,
Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Faith Shayo akizungumza kuhusu
UNESCO inavyoshiriki moja kwa moja kwenye jamii hasa kuzisadia Radio za
kijamii ili kufanya kazi zake kifanisi wakati wa kufunga mafuzo
ya mafundi mitambo kutoka redio jamii 25 zilizopo Tanzania Bara na
Zanzibar yaliyofanyika kwa siku saba katika ukumbi wa Uwanja wa Taifa
jijini Dar es Salaam. Mafunzo haya ya siku saba yameratibiwa na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO).
Kaimu
Mkurugenzi Idara ya Ufundi kutoka TBC, Joseph Kambanga akizungumza
namna TBC ilivyojitolea kuzisaidia Radio za kijamii ili kuimarisha
upatikanaji wa habari na hata kuimarisha mitambo ya urushwaji wa
matangazo kwenye jamii haraka wakati kufunga mafuzo ya mafundi mitambo
kutoka redio jamii 25 zilizopo Tanzania Bara na Zanzibar yaliyofanyika
kwa siku saba katika ukumbi wa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Mratibu
wa Mafunzo kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu,
Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Rose Mwalongo akisisitiza umoja wa mafundi
mitambo waliopata mafunzo ili kuweza kufikia malengo waliyojiwekea
wakati wa kufunga mafunzo hayo.
Fundi
Mitambo wa Redio Jamii Orkonerei FM, Baraka David Ole Maika akitoa
shukrani kwa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu,
Sayansi na Utamaduni (UNESCO) pamoja na Shirika la utangazaji la
Tanzania(TBC) kwa kuweza kutoa mafunzo kwa mafundi mitambo kutoka redio
jamii 25 yalifanyika kwa Siku saba katika ukumbi wa Uwanja wa Taifa
jijini Dar es Salaam.
Mratibu
wa Mafunzo kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu,
Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Rose Mwalongo(wa kwanza kushoto) pamoja
na walimu waliotoa mada mbalimbali katika mafunzo kwa mafundi mitambo
wakiwa kwenye mkutano wa kufunga mafunzo hayo.
Baadhi
ya mafundi mitambo wa radio za kijamii 25 wakifuatilia mada wakati wa
kufunga mafunzo ya kuwajengea uwezo yaliyofanyika kwa siku saba katika
ukumbi wa Uwanja wa Taifa na kuratibiwa na Shirika la Umoja wa Mataifa
linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO).
Kaimu
Mkuu wa Ofisi za Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu,
Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Faith Shayo (kushoto) akiwakabidhi
vyeti baadhi ya mafundi mitambo kutoka radio za kijamii 25 za hapa
nchini. Katikati ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Ufundi kutoka TBC, Joseph
Kambanga.
Kaimu
Mkurugenzi Idara ya Ufundi kutoka TBC, Joseph Kambanga (kushoto)
akiwakabidhi vyeti vya kuhitimu kwa baadhi ya mafundi mitambo kutoka
radio za kijamii 25 kutoka Tanzania Bara na visiwani.
Kaimu
Mkuu wa Ofisi za Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu,
Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Faith Shayo akiwa kwenye picha ya
pamoja na wahitimu ambao ni mafundi mitambo kutoka radio za kijamii 25
mara baada ya kufunga mafunzo hayo yaliyofanyika kwa siku saba.


No comments :
Post a Comment