Na Mahmoud Ahmad Dodoma
Imeelezwa kuwa hapa nchini
TANZANIA hutumia zaidi ya dola milioni 200 sawa na bilioni 400(Mutungi
and Affognon 2013) kuangiza chakula kutoka nje ya nchi kila mwaka hali
inayosabaisha wakulima wadogo wadogo kulazimika kuuza mazao yao kwa bei
ya nchini.
Hayo yalibainishwa mwishoni mwa
wiki na Afisa habari wa wakulima wadogo Tanzania Flora Mlowezi wakati
wa mkutano wa wadau wa sekta ya kilimo na kamati ya bunge kilimo, mifugo
na maji uliofanyika bungeni jijini Dodoma.
Mlowezi alisema wakulima
wanalazimika kuuza mazao kwa bei ya chini kwa sababu ya uwezo mdogo
kwenye usimaminzi wa mazao baada ya mavuno.
Aliongeza kuwa katika Afrika
Mashariki ni asilimia tano tu ambayo huwekezwa kwenye usimaminzi wa
mazao baada ya mavuno na asilimia 95 hutumika katika uzalishaji.
‘’Thamani ya upotevu kwenye nafaka kwa mwaka ni zaidi ya dola milioni nne sawa na bilioni nane (Rockeffer foundation)’’alisema.
Alifafanua kuwa zaidi ya asilimia
70 ya wanawake wa Tanzania wanahusika katika uzalishaji wa mahitaji ya
chakula pia sera ya Taifa ya kilimo ya mwaka 2013 imesema zaidi ya
asilimia 90.4 ya wanawake wa Tanzania wanajihusisha na shughuli za
kilimo na kutimiza lengo namba mbili la ajenda ya malenho endelevu
(2030).
‘’Wengi wao ni wakulima wadogo
ambao hawana uwezo wa kuendesha shughuli za kilimo kwa ufasaha kutokana
na changamoto mbalimbali kama upatikanaji wa pembejeo kwa wakati na kwa
bei nafuu, ukosefu wa taarifa, mitaji na kufikiwa na huduma za ugani
pamoja na uhakika wa ardhi,’’alisema Mlowezi.
Naye msemaji wa shirika lisilo la
kiserikali la Action Aid Joram Wimmo alisema katika bidhaa ya maziwa
bado upo uwezekano wa kuzalisha zaidi kutokana na hivi sasa kuwa katika
kiwango cha chini.
Alisema hivi sasa kuna viwanda 75
vya maziwa vyenye uwezo wa kusindika lita 672,000 kwa siku , uwezo wa
sasa kwa siku ni lita 155,450 sawa na asilimia 23.3 kwa siku.
‘’Maziwa yanayozalishwa ni wastani
wa lita bilioni 2.2 kwa mwaka, kati ya hayo ni asilimia 10 tu ndiyo
yanayoingia katika mfumo rasmi wa soko kutokana na kiasi kidogo
kinachosindikwa nchini bado tunatumia kiasi cha Sh. bilioni 23.6 kuagiza
maziwa nje ya nchi kwa mwaka,’’ alisema Wimmo.
Wimmo aliiomba serikali kutenga
fedha ya kutosha ili kuboresha huduma za ugani na pembejeo ,serikali
kutekeleza miongozo kwa kuzingatia ikama ya kila kijiji kwa kila watu
600 awepo afisa ugani mmoja au zaidi.
Mara baada ya kupokea taarifa hiyo
wabunge wa kamati ya kilimo, mifugo na maji akiwemo mwenyekiti wa
kamati hiyo Christine Ishengoma alisema wameipokea taarifa hiyo na
kuahidi kuifanyia kazi na kuishawishi serikali kuongeza bajeti ili
kuweza kutatua changamoto hizo.
Lengo la mkutano huo ni
kuwasilisha mapendekezo ya wakulima kwa kamati ya kilimo, mifugo na maji
ili waishauri Serikali kutwenga bajeti yakutosha ili kuwepo na
uboreshwaji wa miundombinu kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji.
No comments :
Post a Comment