Waziri wa Elimu Sayansi na
Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akiwasilisha hotuba ya makadirio ya
mapato na matumizi ya Fedha kwa Wizara hiyo kwa mwaka 2018/19 Bungeni
mjini Dodoma mapema leo.
Naibu Waziri wa Nishati Mhe.
Subira Mgalu akitoa maelezo Bungeni mapema leo kuhusu mikakati ya
Serikali kuhusu kufikisha umeme katika vijiji vyote hapa nchini.
Mbunge wa Mwanga Prof. Jumanne
Maghembe akichangia hoja ya Bajeti ya Wizara ya Elimu Sayansi na
Teknolojia kuhusu mikakati inayoweza kusaidia kuendelea kukuza kiwango
cha elimu hapa nchini.
Naibu Waziri wa Ujenzi Uchukuzi
na Mawasiliano Mhe. Elias Kuandikwa akijibu swali Bungeni mjini Dodoma
kuhusu hatua zinazochukuliwa na Serikali katika kujenga miundo mbinu
hapa nchini.
Wageni mbalimbali walihudhuria
Bunge wakiwemo Skauti wakifuatilia kipindi cha maswali na majibu mapema
leo Bungeni mjini Dodoma.
Naibu Waziri wa Fedha Dkt. Ashatu
Kijaji akisisitiza jambo kwa Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi
Isack Kamwelwe leo mjini Dodoma.
(Picha zote na MAELEZO
No comments :
Post a Comment