Na.Vero Ignatus Arusha.
Wafanyakazi watano wa Mamlaka ya Hifadhi ya
Ngorongoro(NCAA])wamefikishwa mahakamani leo kwa kosa la kuisababishia hasara serikali na kusababisha hasara ya dola za Kimarekani 35,500.
Ngorongoro(NCAA])wamefikishwa mahakamani leo kwa kosa la kuisababishia hasara serikali na kusababisha hasara ya dola za Kimarekani 35,500.
Watuhumiwa
waliofikishwa kizimbani na kukabilia na shitaka moja ni pamoja na
Joseph Mtwala{36},John Mlambo{42},Mwahu Yunus {38},Mery Njau{38} na
Catherini Edward {33}.
Watuhumiwa
hao wote kwa pamoja walisomewa shitaka moja na Mwendesha Mashitaka wa
Taasisi ya Kuzuia na Kupamba na Rushwa{TAKUKURU} ,Adamu Kilongozi akiwa na Hamidu Simbano na Richard Jacopiyo kuwa walitenda kosa hilo kati ya desemba 25 mwaka 2013 na juni 6 mwaka 2014.
Kilongozi
alidai mahakamani hapo kuwa watuhumiwa hao wakiwa katika lango la Nabi
Mkoani Mara na lango kuu la Loduare Mkoani Arusha watuhumiwa hao
walisababishia serikali hasara ya fedha za Kimarekani kiasi hicho wakiwa
watumishi wa NCAA.
Mwendesha mashitaka huyo alisoma shitaka hilo mbele ya Hakimu mkazi wa mahakama ya wilaya ya Arumeru Mkoani Arusha,Bernad Nganga na kueleza kuwa walifanya kosa hilo huku wakijua ni kinyume na sheria.
Watuhumiwa
wote walikana shitaka hilo na walipewa dhamana ya fedha taslimu
shilingi milioni 7.9 au mali isiyohamishika yenye thamani hiyo na
taratibu za dhamana zilikuwa zikiendelea .
Mwendesha
mashitaka wa TAKUKURU alisema kuwa ushahidi wa kesi hiyo umekamilika na
aliiomba mahakama hiyo kupanga Tarehe ya kuanza usikilzwaji wa awali
Watuhumiwa wote watano wamepelekwa rumande kwakushindwa kukidhi masharti ya dhamani ,ambapo watasomewa hoja za awali April 10 mwaka huu.

No comments :
Post a Comment