
Waziri Jafo akigawa zawadi ya mipira kwa baadhi ya shule za sekondari zitakazoshiriki.
Waziri wa TAMISEMI, Selemani Jafo akihutubia wakati wa uzinduzi huo.
Meneja wa chapa ya Coca-Cola, Sialouise Shayo, akiongea wakati wa uzinduzi huo.

Waziri Jafo akikagua moja ya timu na kugawa vifaa kwa baadhi ya shule za sekondari

Waziri Jafo akikagua moja ya timu na kugawa vifaa kwa baadhi ya shule za sekondari
Waziri Jafo katika picha ya pamoja na wadau mbalimbali wa UMISSETA baada ya uzinduzi.
Wakazi wa Dodoma walijitokeza kushuhudia uzinduzi.
Mashindano ya shule za sekondari
ya UMISSETA ngazi ya mkoa yamezinduliwa mkoani Dodoma, na mgeni rasmi
katika uzinduzi huo alikuwa ni Waziri wa TAMISEMI,Selemani Jafo.Uzinduzi
huo pia ulihudhuriwa na wanafunzi wa shule za sekondari,walimu,
viongozi mbalimbali wa mkoa na michezo.
Mbali na uzinduzi,Waziri
alikabidhi vifaa vya michezo kwa timu za sekondari zilizokuwepo kwenye
uzinduzi huo.Vifaa hivyo vya michezo vimetolewa na kampuni ya Coca-Cola
ambayo
ni mdhamini mkuu wa mashindano haya,ambapo mwaka huu imepanga
kutoa vifaa vya michezo kwa shule 4,000 za sekondari zilizopo sehemu
mbalimbali nchini.
Waziri Jafo, alisema kampuni ya
Coca-Cola kwa kudhamini mashindano hayo kutafanikisha jitihada za
kuendelea kuibua vipaji vya wachezaji chipukizi wa michezo ya soka
,mpira wa kikapu na pia kupitia mashindano haya kutaibuliwa vipaji vya
wanariadha watakaotamba katika kipindi cha miaka ijayo.
“Nafahamu kuwa udhamini wa
Coca-Cola wa mashindano haya unamalizika mwishoni mwa mwaka huu,lakini
natoa ombi maalum iangalie uwezekano wa kuendelea kuongeza kipindi cha
kutoa udhamini .Mashindano haya ya UMISSETA ni tanuru ya kuibua vipaji
na rekondi ipo ya wachezaji wazuri wa soka waliofanya vizuri na
wanaoendelea kufanya vizuri katika michezo mbalimbali,vipaji vyao
viliibuliwa katika mashindano haya wengi pia wamechezea baadhi ya klabu
kubwa za soka za Yanga na Simba”alisema.
Waziri Jafo,alitoa wito kwa
makampuni mengine kujitokeza kudhamini mashindano ya michezo kuanzia
ngazi za chini,na kusisitiza kuwa sekta ya michezo inazidi kukua ambapo
hivi sasa lengo lake sio burudani bali ni biashara kubwa na ushahidi wa
suala hili upo wazi.
Jafo pia alishauri kamati ya
maandalizi ya mashindano haya ya UMISSETA ,kwa miaka ijayo ihakikishe
uzinduzi wake ngazi ya kitaifa unafanyika mkoani odoma badala ya mkoani
Mwanza ili yaendane na mkakati wa serikali ya awamu ya tano chini ya
Rais John Magufuli ya kuhamishia shughuli za serikali katika mji wa
makao makuu ya nchi.
Kwa upande wake Meneja wa chapa ya
Coca-Cola, Sialouise Shayo,alisema kampuni ya Coca-Cola inajivunia kuwa
mdhamini wa mashindano haya kwa kipindi cha miaka 3 mfulilizo na
inaamini vipaji vingi vimeibuliwa na vitaendelea kuibuliwa .”Udhamini
wetu katika mashindano haya tumejikita katika kutoa vifaa vya michezo
kwa wachezaji wanaoshiriki kuanzia ngazi ya mkoa hadi ngazi ya
taifa,kutoa mafunzo kwa makocha wanaofundisha timu na zawadi kwa timu
zinazofanikiwa kufanya vizuri”,alisisitiza
Shayo alisema mbali na uzinduzi wa
UMISSETA ngazi ya mkoa uliofanyika mkoani Dodoma utafanyika katika
mikoa ya Kagera,Tanga,Mtwara,Singida na Zanzibar ambapo uzinduzi kwa
ngazi ya taifa utafanyika mkoani Mwanza ambapo pia mashindano haya
yatafanyika.




No comments :
Post a Comment