Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri
Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista
Mhagama akiwasilisha Taarifa ya Utekelezaji wa Bajeti ya Ofisi ya Waziri
Mkuu kwa mwaka 2017/18 na Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka
2018/19 kwa mafungu 25 na 37 Kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na
Sheria Machi 27, 2018 Bungeni Dodoma.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya
Katiba na Sheria Mhe.Najma Giga akiongoza kikao cha kamati yake wakati
wa Uwasilishaji wa Taarifa ya Utekelezaji wa Bajeti ya Ofisi ya Waziri
Mkuu kwa mwaka 2017/18 na Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka
2018/19 kwa mafungu 25 na 37 Bungeni Dodoma.
Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya
Kudumu ya Katiba na Sheria wakifuatilia kikao cha kujadili Makadirio ya
Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa Mwaka 2018/2019 kilichofanyika Mjini
Dodoma.
Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya
Kudumu ya Katiba na Sheria wakifuatilia kikao cha kujadili Makadirio ya
Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa Mwaka 2018/2019 kilichofanyika Mjini
Dodoma.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu
(Bunge na Waziri Mkuu) Bi. Maimuna Tarishi akifuatilia uwasilishwaji wa
makadirio ya bajeti ya Ofisi yake wakati wa kikao cha Kamati ya Kudumu
ya Katiba na Sheria Kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Sera na Mipango ofisi
hiyo Bw.Packshard Mkongwa.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri
Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista
Mhagama akiwasilisha Taarifa ya Utekelezaji wa Bajeti ya Ofisi ya Waziri
Mkuu kwa mwaka 2017/18 na Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka
2018/19 kwa mafungu 25 na 37 Kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na
Sheria kilichofanyika Machi 27, 2018 Bungeni Dodoma.
Mmoja wa wajumbe wa Kamati ya
Kudumu ya Katiba na Sheria Mhe.Amina Mollel akiuliza swali wakati wa
kikao cha kamati hiyo kilichofanyika Machi 27, 2018.
Mmoja wa wajumbe wa Kamati ya
Kudumu ya Katiba na Sheria Mhe.Saed Kubenea akiuliza swali wakati wa
kikao cha kamati hiyo kilichofanyika Machi 27, 2018.
Mkurugenzi wa Uendeshaji wa WCF
Bw.Anselim Peter akiwasilisha mada kuhusu Utekelezaji wa sheria ya fidia
kwa wafanyakazi kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na
Sheria Machi 27, 2018.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu
(Kazi, Ajira na Vijana), Mhe. Antony Mavunde akizungumza jambo wakati wa
kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria kilichofanyika
mjini Dodoma.
Makatibu Wakuu Ofisi ya Waziri
Mkuu wakiteta jambo mara baada ya kumaliza kikao cha Kamati ya Kudumu ya
Katiba na Sheria, wa kwanza kushoto ni Katibu Mkuu (Sera na Uratibu)
Prof.Faustin Kamuzora, Katikati ni Bi.Maimuna Tarishi (Bunge na Waziri
Mkuu) na wa kwanza kulia ni Bw. Erick Shitindi (Kazi, Vijana, Ajira na
Wenye Ulemavu)
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri
Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista
Mhagama (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Watumishi
wa ofisi hiyo mara baada ya kikao cha Kamati ya Kudumu ya Katiba na
Sheria kupitisha Makadiri ya bajeti ya Ofisi yake kwa mwaka 2018/19 kwa
Fungu 25 na 37 Dodoma.
(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU – DODOMA
…………………
Na MWANDISHI WETU
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge, Kazi,Vijana, Ajira na
Watu wenye Ulemavu Mhe.Jenista Mhagama ameeleza kuwa uwepo wa Mfuko wa
Fidia kwa Wafanyakazi ni suala muhimu kuzingatia faida nyingi zitokanazo
na mfuko huo tofauti na ilipokuwa awali.
Ameyasema hayo leo mjini Dodoma
wakati wa Uwasilishaji wa Taarifa ya Utekelezaji wa Bajeti ya Ofisi ya
Waziri Mkuu kwa mwaka 2017/2018 na Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa
mwaka 2018/2019 kwa mafungu 25 na 37 kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya
Katiba na Sheria.
Waziri Mhagama alieleza kwamba,
miongoni mwa faida za uwepo wa mfuko huo ni pamoja na wafanyakazi kuwa
na maisha bora kutokana na muendelezo wa kipato baada ya kupata ajali au
kupoteza uwezo wa kufanya kazi, mazingira bora na yenye uhakika kazini
na waajiri kupata unafuu wa kulipa gharama mbalimbali endapo mfanyakazi
atapata janga kazini kwa sasa mzigo huu unabebwa na mfuko na kuwa na
ongezeko la tija kazini kutokana na wafanyakazi kufanya kazi kwa ari
pamoja na kuwepo kwa wingi kazini.
“Hakika mfuko huu ni mkombozi
mkubwa kwa wafanyakazi na waajiri wote kwa kuzingatia umekuja wakati
mwafaka na umeongeza tija kwa kuwa malengo ya mfuko yanapelekea maisha
bora kwa wafanyakazi na kuleta tija kuzingatia umuhimu wake”.Alisema
Mhagama
Pamoja na hayo Waziri Mhagama
aliwapongeza WCF kwa hatua nzuri ya kuanzisha mfuko huo wenye malengo
chanya yatayosaidia kuongeza na kuendeleza azma ya Serikali ya kuwa na
Uchumi wa Viwanda kwa kuwa wafanyakazi watakuwa na mazingira mazuri ya
uzalishaji na ukuzaji wa uchumi wa nchi.
“Kipekee niwapongeze WCF kwa kuwa
na mfuko huu, tunapaswa kuhakikisha unakuwa endelevu na wa mfano kwani
unasaidia kuleta chachu katika ukuaji wa uchumi na kuisaidia Serikali
kufikia azma yake ya kuwa na Uchumi wa Viwanda”.Alisisitiza Mhagama
Naye Mkurugenzi wa Uendeshaji wa
WCF Bw.Anselim Peter alieleza kuwa, mfuko unamajukumu mengi yenye
malengo chanya ikiwemo kusaidia kubuni, kukuza na kuendeleza mbinu za
kupunguza ajali katika maeneo ya kazi.
“Miongoni mwa majukumu ya mfuko
huu, haikuwa kulipa fidia pekee bali kuwa na mbinu mbalimbali za
kibunifu za kupunguza au kumaliza kabisa ajali katika maeneo ya
kazi”.Alisisitiza Anselim.
Aliongeza kuw, kufanikisha hayo
yote,michango ya wabunge ni muhimu katika kutoa uelewa sahihi wa
madhumuni na uendeshwaji wa mfuko huo.
Kwa upande wake mmoja wa wajumbe
wa Kamati ya Katiba na Sheria Mhe.Saed Kubenea (Mb) alipongeza kazi
nzuri inayofanywa na mfuko na kuwaomba kuwa pamoja na mfuko kujali
wafanyakazi wawapo kazini ni vyema pia kuendelea kuhamasisha zaidi kwa
kutoa elimu juu ya mfuko ili umma wa Watanzania kuelewa faida za mfuko
huo.
AWALI
Workers Compensation Fund
(WCF) ni Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi wa Sekta ya Umma na Binafsi
uliochini ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu
na umeundwa kwa mujibu wa kifungu cha 5 cha sheria ya Bunge ya Fidia kwa
wafanyakazi namba 20 ya mwaka 2008 ukiwa na wajibu wa kutoa Mafao ya
Fidia kwa mfanyakazi apatwapo na madhara mahala pa kazi.
No comments :
Post a Comment