Kamanda wa polisi
Mkoani Pwani ,(ACP) Jonathan Shanna akizungumza na waandishi wa habari
ofisini kwake (hawapo pichani).(picha na Mwamvua Mwinyi
…………………
Na Mwamvua Mwinyi,Kibaha
JESHI la polisi
mkoani Pwani, linawashikilia watu wawili wanaodaiwa kuwa ni majambazi
kati ya kundi la majambazi zaidi ya sita ambao waliteka magari na kupora
mali mbalimbali za watu eneo la Kwang’andu ,Mbwewe barabara ya kuelekea
Wami.
Kamanda wa polisi mkoani Pwani,(ACP) Jonathan Shanna alisema tukio hilo limetokea machi 24 saa 8.30 mchana .
Akizungumzia tukio
hilo la unyanga’anyi wa kutumia silaha ,alieleza majambazi zaidi ya sita
waliteka magari kwa kukata mti kwa msumeno kisha kuziba barabara na
kuvamia magari mbalimbali ya wananchi kisha kuwapora mali zao na
kuharibu baadhi ya magari yao.
Aidha kamanda Shanna alisema, watuhumiwa wawili wapo mbaroni kupisha uchunguzi.
Aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Saidi Salim (26) na Nyangwesa Nyangwesa.
Kamanda Shanna
aliwataja na wananchi /wasafiri walioharibiwa na kuporwa mali zao
akiwemo Peter Kilango, ambae aliporwa simu aina ya techno C9 na gari
lake kuharibiwa kioo cha mbele upande wa dereva.
Viatus Bahati
aliporwa Lap Top Dell, Usd 900.00 , shilingi 700,000 na pochi yenye
document mbalimbali na Imail Meshileki alieporwa simu aina ya Tecno ,na
sh .800,000 na gari lake T.953 BXN Toyota Prado ambayo waliiharibu kioo
cha nyuma.
Kamanda Shanna
alimtaja mwingine ni Jackson Omary aliyeporwa Tsh.70,000 na begi lenye
nguo mbalimbali na Denis Mwavano aliporwa simu Tecno C9.
Jeshi la polisi
mkoani humo limekemea vitendo vya kiuhalifu na kuteka magari kwani kwa
kufanya hivyo watakula nao sahani moja ,na wale waliofanikiwa kukimbia
wataendelea kusakwa.
No comments :
Post a Comment