Thursday, March 1, 2018

KUJISAJILI WCF LENGO NI KUMUONDOLEA MZIGO WA GHARAMA MWAJIRI NA KULINDA HAKI ZA MFANYAKAZI: MAVUNDE

 NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID, MOSHI
SERIKALI ya awamu ya tano
imedhamiria kwa dhati kuhakikisha wafanyakazi wanalindwa na kupata haki zao
pindi wanapopatwa na madhara yatokanayo na kazi, Naibu Waziri  Ofisi ya
Waziri Mkuu, anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Antony Mavunde
amesema mjini Moshi Mkoani Kilimanjaro..

 Mheshimiwa
Mavunde ameyasema hayo jana (Machi 1, 2018), wakati akiendelea na ziara yake ya
kushtukiza ili kuwabaini waajiri ambao bado hawajatekeelza takwa la kisheria
linalowataka waajiri wote katika sekta rasmi,(umma na binafsi), waliopo
Tanzania Bara kujisajili na kuchangia kwenye Mfuko huo.

Kwa mujibu wa Sheria
iliyoanzisha Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, Ikiwa Mwajiri hatajisajili kwenye
Mfuko, atakuwa ametenda kosa la jinai kwa mujibu wa kifungu cha 71(4) cha
Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi na akipatikana na hatia adhabu yake ni kulipa
faini isiyozidi shilingi milioni 50,000,000 (Milioni Hamsini) au kifungo
kisichozidi miaka mitano jela au adhabu zote kwa pamoja, alisema Mhe. Mavunde.

 Mheshimiwa Mavunde
ambaye alifuatana na Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Mfuko huo Bw. Anslem Peter na
Kaimu Kamishna kutoka Idara ya Kazi, Bi. Rehema Moyo, alibaini Mkoa wa
Kilimanjaro wenye jumla ya Waajiri 1,039 ni waajiri 525 tu ndio wamejisajili
huku wengine 514 bado hawajajisajili na Mfuko.

 “Serikali ilikwishatoa
matamko mbalimbali yanayowahimiza waajiri kutekeleza takwa hilo la kisheria, na
leo hii hakuna njia nyingine, Waajiri hawa tuliowabaini hapa Mkoani Kilimanjaro
naagiza WCF iwapeleke mahakamani haraka iwezekanavyo ili sheria ichukue mkondo
wake.” Alisema.

Baadhi ya waajiri ambao
Naibu Waziri na timu yake walifanya ukiaguzi huo ni pamoja na kampuni ya
Machare Investments, Scholastica Schools iliyoko Himo nje kidogo ya mji wa
Moshi.

 Alisema sio lengo la
serikali kuwatisha au kuwadhalilisha waajiri hao bali nia ni kuhakikisha haki
za wafanyakazi zinalindwa lakini pia kuwaondolea jukumu waajiri la kuwahudumia
wafanyakazi wao wanapopatwa na madhara wakiwa kazini.

 “Tunataka
ninyi wawekezaji, (waajiri), mjielekeze kwenye shughuli zenu za msingi kwa
maana ya kufanya uwekezaji na biashara zenu na hili la kumuhudumia mfanyakazi
aliyepatwa na madhara kazini lishughulikiwe na serikali.” Alisisitiza.

Tayari
Mhe. Mavunde amefanya ziara kama hiyo mkoani Mwanza na Shinyanga na kubainisha
kuwa operesheni hiyo ya kuwabaini waajiri wasiotekeleza takwa hilo la kisheria
litafanyika nchi nzima, na kuwataka waajiri kufanya hivyo haraka ili wasijikute
kwenye matatizo.

“Tumewasambaza
maafisa wetu wa WCF mikoani na wanaednelea na utaratibu wa kuwafuikisha
mahakamani waajiri wote ambao wameshindwa kufuata sheria.
Naibu Waziri ya
Waziri Mkuu, anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Antony Mavunde(katikati), akiongozana na Mkurugenzi wa Uendeshaji WCF, Bw. Anslem Peter, (kulia) na Mhasibu wa Shule ya Scolastica, Bw.Moshi W.Moshi, wakati wa ziara yake ya kushtukiza shuleni hapo ili kubaini waajiri ambao hawajajisajili na Mfuko wa Fidia Kwa wafanyakazi, (WCF) ambapo ilibainika shule hiyo kubwa mjini Moshi haijatekeleza takwa hilo la kisheria
Mhaisbu wa Shule ya Scolastica mjini Moshi, Kilimanjaro Bw. Moshi W. Moshi, na Mkuu wa shule hiyo Bw.Michael Shiloli, wakisikilzia maagizo ya Naibu Waziri Mvunde.

 Mkurugenzi  wa Uendeshaji WCF, Bw. Anselim Peter, (kulia), akijadili jambo na Kaimu Afisa Kazi Mkoa wa Kilimanjaro, Bi.Neema Msyalika na Afsia Mwandamizi wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano WCF, Bw. Sebere Fulgance.
 Mhe. Mavunde akizungumza na Mkurugenzi wa Machare Investments, (kulia)

 

 Bw. Anselim Peter akizungujza na waandishi wa habari
 Mhe. Mavunde akisisitiza jambo kwa viongozi wa shule ya Scolastica.
Mkurugenzi  wa Uendeshaji WCF, Bw. Anselim Peter, (kulia), akijadili jambo na Kamishna wa kutoka Idara ya Kazi, Bi. Rehema Moyo, (katikati), na   Kaimu Afisa Kazi Mkoa wa Kilimanjaro, Bi.Neema Msyalika 

No comments :

Post a Comment