Kongamano
la biashara lililoandaliwa na Chemba ya Biashara, Viwanda na Kilimo
(TCCIA) limefanyika jijini Dar es salaam na kuzungumzia mambo kadha wa
kadha hususani fursa katika bomba la mafuta la Tanga hadi Hoima, Huduma
za fedha kurahisisha biashara za kimataifa na pia makubaliano ya
biashara kati ya TCCIA na Chemba ya biashara kutoka China.
Akizungumza
wakati wa kufungua rasmi kongamano hilo Charles Itembe ambaye ni
Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Azania alisema “ ikiwa wafanyabiashara
watatumia huduma za fedha za kimataifa kama Letter of Credit basi
itapunguza utapeli na hivyo kukuza biashara. Pia alielezea jinsi benki
ya Azania ilivyo tayari kushirikiana na wafanya biashara katika kukuza
biashara na uchumi wa viwanda”Nae Mwenyekiti wa Infotech group Ali
Mfuruki aliwaasa wafanya biashara kujenga viwanda vyenye kusaidia lengo
la Serikali la kuhakikisha viwanda vinajengwa.
Makamu wa Rais wa TCCIA Octa Mshiu alishukuru wanachama wa TCCIA na waalikwa kwa kufika na kibadilishana uzoefu na changamo.Mkurugenzi
Mtendaji wa EAG Group ambao ndio waandaaji wa kongamano hilo kwa
kushirikiana na TCCIA,Imani Kajula “ alisema mkutano huu ni mwendelezo
wa lengo la TCCIA kuwawezesha wanachama wake kuwa na jukwaa la
mashauriano.



No comments :
Post a Comment