Na Masanja Mabula -Pemba ..
WATU
wawili wakaazi wa Mkoa wa Tanga wanashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa
wa Kaskazini Pemba baada ya kukamatwa wakiwa na mafurushi ishirini na
tano (25) ya majani makavu yanayosadikiwa kuwa ni bangi yenye uzito wa
kilo tano na nusu.
Wawili
hao ambao wako chini ya ulinzi wa Polisi la Polisi ni Seif Yussuf
Msumari pamoja na Shadia Stephano wako wakaazi wa Mkoa wa Tanga.
Akizungumza
ofisini kwake Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kaskazini Pemba Kamishna
msaidizi Haji Khamis Haji amesema watuhumiwa hao wamekamatwa na askari
katika eneo la
bandari ya wete.
Amesema
kuwa jeshi la polisi bado linaendelea kuwahoji watuhumiwa na upelelezi
ukikamilika watfikishwa mahakamani kujibu tuhuma ambazo zinawakabili .
“Kwa
sasa tunaendelea kuwahoji na upelelezi ukikamilika watafikishwa
mahakamani kujibu tuhuma ambazo zinawakabili ” alifahamisha.
Amesema
kwa upande wa Jeshi la polisi wamejipanga kuendesha misako na
operesheni sehemu za bandari , madago pamoja na maeneo mengine
yanayodhaniwa kutumika kupitisha dawa za kulevya ili kuweza kutimiza
lengo la kutokomeza biashara haramu ya dawa za kulevya.
“Hizi
operesheni tunazoendelea nazo ni endelevu , lengo ni kuhakikisha
wananchi wanaishi salama bila ya kutumia dawa za kulevya ”alieleza
Kamanda.
Aidha
kmanda haji amewataka wananchi kuendelea kushirikiana na jeshi la
polisi kwa kutoa taarifa sahihi ambazo zitafanikisha kuwakamata
wanaojihusisha na biashara ya dawa za kulevya .
Amesema
jeshi la polisi linahitaji ushirikiano kutoka kwa wananchi pamoja na
vikosi vyengine vya ulinzi katika kufanikisha azma ya kukabiliana na
biashara hii , hivyo ni vyema kila mmoja akatambua kwamba vita ya dawa
za kulevya ni ya wote.
No comments :
Post a Comment