Waziri Waziri Kindamba Mkurugenzi
MKuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL CORPORATION) akizungumza
na waandishi wa habari katika makao makuu ya shirika hilo Jengo la
Extelecoms Mtaa wa Samora jijini Dar es salaam kulia ni Bw.Ali Mbega
Mkuu wa Mauzo na Masoko (TTCL CORPORATION)
Waziri Waziri Kindamba Mkurugenzi
MKuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL CORPORATION)akimzikiliza
Ali Mbega Mkuu wa Mauzo na Masoko (TTCL CORPORATION) wakati alipokuwa
akijibu moja ya swali yaliyoulizwa na waandishi wa habari katika mkutano
huo.
Waziri Waziri Kindamba Mkurugenzi
MKuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL CORPORATION)akijibu
maswali katika mkutano huo pamoja na Ali Mbega Mkuu wa Mauzo na Masoko
(TTCL CORPORATION) na maafisa wengine wa shirika hilo.
……………………………………………………………………………..
Waziri Waziri Kindamba
Mkurugenzi Mkuu wa (TTCL CORPORATION) leo amezindua huduma mpya ya
kampuni hilyo iliyopewa jina la Fiber Connect Bundle, Amesema huu ni
mwendelezo wa ubunifu wa Kampuni yenu ya kizalendo katika kuwapatia
huduma za kipekee kabisa.
Kindamba amesema TTCL Corporation
imechukua hatua ya kuwafuata nyumbani na kufanya mapinduzi makubwa ya
kimawasiliano. Kupitia huduma hii mpya ya Fiber Connect Bundle, ambapo
mteja atapata huduma nne kwa pamoja zikiwa na unafuu mkubwa wa gharama
na ubora wa hali ya juu.
Amesema kwa kuanzia, mradi
unatarajiwa kufikisha huduma katika nyumba zipatazo 500 katika eneo la
Mikocheni, Nyumba 500 zingine katika eneo la Mbezi Beach na nyumba
zaidi ya 200 katika eneo la Medeli Mkoani DODOMA.
Ameongeza kwamba Kupitia
kifurushi cha Fiber Connect, Mteja ataweza kufaidika na huduma
zifuatazo; Kwanza, Mteja atapata Intaneti yenye kasi isiyo na kikomo(
Unlimited). Pili, Mteja atapata huduma ya simu za sauti kwa simu za
mezani na (Sim Card) ambayo ataitumia kwenye simu yake ya mkononi na
kupata huduma ya Intaneti sawa na simu ile anayopata katika simu ya
mezani.
Akizungumzia mwelekeo wa
utendaji wa Shirika amesema unaonesha ukuaji mzuri licha ya changamoto
zilizopo. Mapato yameendelea kuongezeka na hasara kupungua kwa kiasi
kikubwa, jambo linalotupa uhakika wa kutimiza ahadi yetu ya kutoa gawio
Serikalini katika mwaka huu wa fedha 2017/2018.
“Mtakumbuka kuwa, kwa zaidi ya
miaka kumi na tano iliyopita, TTCL haikuawahi kutoa gawio. Tumedhamiria
kuvunja mwiko huu kwa kutimiza ahadi yetu kwa Umma ya kutoa gawio la
shilingi Bilioni moja katika mwaka huu wa fedha” Aemesema Kindamba.
Menejimenti itaendelea kuweka
mkazo katika kuboresha eneo la Huduma kwa Wateja kwa kutoa huduma bora
kwa gharama nafuu, kuongeza Wateja wapya, kusambaza huduma za 4G LTE
katika Makao Makuu ya Mikoa yote Nchini ifikapo Juni 2018.
Aidha, tutaendelea kuongeza
uwekezaji katika Teknolojia na Miundo mbinu yetu kote nchini, kuboresha
mazingira ya kazi kwa Wafanyakazi na Vitendea kazi, kukusanya Madeni ya
Shirika, kuongeza Wateja na ufanisi katika huduma za fedha Mtandao (TTCL
PESA) na kuongeza ufanisi katika Miundombinu ya Kimkakati ya Serikali
inayosimamiwa na kuendeshwa na Shirika la Mawasiliano Tanzania na hapa
ninazungumzia Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano (NICTBB) na Kituo Mahiri
cha kuhifadhia Kumbukumbu(National Data Centre).
Huduma ya tatu , Mteja atapata
huduma za wireless service (WiFi) katika nyumba yake ambapo vifaa vyote
vinavyotumia Teknolojia ya Intaneti vitaunganishwa na kuweza kutumia
huduma hii. Mfano wa vifaa husika ni Smart Tv, Tablets, Laptops na
kadhalika
Nne, Mteja atapatiwa vifaa vyote bure pamoja na uhakika wa huduma za baada (After Sells Services) endapo itahitajika
Mchanganuo wa gharama na mgawanyiko wa kifurushi hiki ni kama ifuatavyo
Jina la Kifurushi | Muunganiko wa Huduma | Gharama | Matumizi | |
Kasi ya Intaneti (Mbps) | Dakika za maongezi Mitandao yote | |||
Fiber Connect Lite | 10 | 50 | 100,000.00 | Siku 30 |
Fiber Connect Basic | 30 | 100 | 150,000.00 | |
Fiber Connect Preffered | 50 | 300 | 200,000.00 |
Ili kupata huduma ya kifurushi
hiki maalumu cha FTTH, Mteja unapaswa kufanya yafuatayo; Piga namba 100/
022214100100 kuongea na Wahudumu wetu au
Tembelea kituo chetu cha Huduma kwa Wateja kilicho karibu nawe.
Huduma hii inazilenga: Taasisi zote za Serikali, Wafanyabiashara wakubwa, wa kati na wadogo na Ofisi mbalimbali.
No comments :
Post a Comment