Mkuu wa
Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo amewaasa watumishi wa amshirika ya
umma na wakala wa serikali mkoani Rukwa kutotumia vyeo vyao kuwanyanyasa
wananchi wanaowahudumia na badala yake wawasaidie kwa kuzingatia
misingi ya haki na usawa bila ya kujali, rangi kabila, dini na hali zao
kiuchumi.
Amesema kuwa watumishi wa serikali ni watumishi wa
wananchi hivyo wanapaswa kujituma bila ya kujali vyeo vyao kwani vyeo
hivyo havitakuwa na maana ikiwa wananchi hawapati huduma wanayoitarajia
kutoka katika serikali waliyoiweka madarakani.
“Sisi viongozi wa
Serikali lazima tufanye kazi kwa kujituma na kujitoa na tukumbuke kuwa
sisi ni watumishi tu, sio watu wa kujivuna ama wabinafsi na kujinadi kwa
vyeo vyetu kwamba mimi meneja, daktari sijui nani, vyeo vyetu vitakuwa
na maana pale tu tunapokwenda kwa wananchi na kuwapa huduma” Alieleza.
Na
kuongeza kuwa serikali ya awamu ya tano ipo kuhakikisha kuwa kila
kiongozi anayehudumia wananchi anakuwa mtumishi wa wananchi na
kuhakikisha kuwa haki inatendeka na kuonya vikali watumishi
wanaowahudumia wananchi kwa kutumia lugha chafu.
Ameyasema
hayo kwenye kikao cha muda mfupi kilichowajumuisha viongozi kutoka
katika mashirika ya umma, wakala na mamlaka mbalimbali za serikali
zilizomo Mkoani humo ili kufahamu matatizo wanayokumbana nayo pindi
wanapotimiza wajibu wao wa kuwahudumia wananchi.
Sambamba na hayo
Mh. Wangabo amewataka watumishi wote Mkoani humo kuzingatia muda na
kutekeleza kwa wakati mipango waliyojiwekea ili kazi zizae matunda na
kutoa taarifa sehemu husika bila ya kusubiri kusukumwa.
Mkuu wa
Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo akifafanua namna mtumishi anavyotakiwa
kuwajibika pindi anapowahudumia wananchi (aliyekaa) kaimu Katibu
Tawala Mkoa wa Rukwa David Kilonzo.
Viongozi
wa mashirika ya ya umma na mamlaka mbalimbali za seikali Mkoani Rukwa
Waliohudhuria kwenye kikao hicho kilichowakutanisha wakuu wa mamlaka na
mashirika ya
Pages
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)


No comments :
Post a Comment