Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo
ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile akizungumza
wakati wa hafla ya uzinduzi wa Cheti cha Mfumo wa Uhakiki Ubora wa
Huduma cha Kiwango cha Kimataifa (ISO 9001:2015) leo Jijini Dar es
Salaam. TFDA imekuwa ya kwanza miongoni mwa mamlaka zinazoshughulika na
...
udhibiti wa ubora wa chakula na dawa katika ukanda wa Afrika Masharika
kutunikiwa cheti hicho.
…………………………………………………………………………………..
Na: Frank Shija- MAELEZO
NAIBU Waziri wa Afya, Maendeleo
ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile ameipongeza
Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA) kuwa Mamlaka ya kwanza
inayojishugulisha na udhibiti ubora wa chakula na dawa katika ukanda wa
Afrika Mashariki kutunukiwa Cheti cha Mfumo wa Uhakiki Ubora wa Huduma
cha Kiwango cha Kimataifa (ISO 9001:2015).
Akzungumza katika uzinduzi wa
Cheti hicho leo Jijini Dar es Salaam, Dkt Ndugulile alisema cheti hicho
cha ubora ni kielelezo cha Taasisi hiyo kusimamia misingi ya ubora
katika utendaji kazi wake katika Mfumo wa uhakiki ubora wa huduma katika
kiwango cha Kimataifa.
Ðk. Ndugulile amesema kuwa
mafanikio hayo ya TFDA ni matokeo ya utekelezaji wa azma ya Serikali ya
Awamu ya Tano katika kuhakikisha huduma bora za afya hususani katika
udhibiti na upatikanaji wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi.
“Utekelezaji wa mfumo huu na
kupatikana kwa cheti hiki ni ishara nzuri kwamba TFDA inasimamia vyema
mifumo yake ya kiutendaji ili kuhakikisha huduma zitolewazo zina ubora
na zinakidhi matakwa ya kiwango cha Kimataifa cha ISO 900: 2015, hii pia
inaleta imani kubwa kwa sisi tunaowasimamia utendaji wenu na wananchi
wanaotumia bidhaa mnazozidhibiti kwa ujumla,” Alisema Dkt. Ndugulile.
Naye Mkurugenzi Mkuu wa TFDA,
Hiiti Sillo alisema mamlaka hiyo imetunukiwa cheti hicho kimeifanya
taasisi hiyo kuwa Mamlaka ya kwanza miongoni mwa mamlaka zinazojihusisha
na udhibiti wa ubora wa chakula na dawa katika ukanda wa Afrika
Mashariki na ya pili kwa nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara.
Aliongeza kuwa TFDA imekuwa
ikitekeleza Mfumo wa Uhakiki Ubora wa Huduma kuanzia mwaka 2005 baada ya
kufanya tathmini ya namna bora ya kufanya shughuli za udhibiti kwa
ufanisi na kutoa huduma bora kwa wateja.
“Katika kuendelea kukidhi
matarajio ya wateja na kuendana na matakwa ya wateja wetu na wadau kwa
ujumla, tuliamu kuboresha Mfumo wetu wa Uhakiki Ubora wa Huduma ili
uendane na matakwa ya kiwango kipya cha Kimataifa, tulifanikiwa
kutunukiwa cheti cha ISO 9001:2015 baada ya ukaguzi wa kina mnamo mwezi
Agosti mwaka huu,” alisema Mkurugenzi Sillo.
No comments :
Post a Comment