Waziri wa Nishati wa Tanzani,
Dkt. Medard Kalemani (kulia) na Waziri wa Nchi anayeshughulikia
Nishati kutoka nchini Uganda, Dkt. Simon Du’ Ujanga wakitia saini
ripoti ya mkutano huo. Wanaoshuhudia wa kwanza kushoto ni Naibu Katibu
Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki upande wa Sekta za Kijamii na
Uzalishaji, Christophe Bazivamo na wawakilishi wa Mawaziri wa nchi
wanachama.
Makatibu Wakuu wa nchi wanachama
wakisaini ripoti iliyojadiliwa katika mkutano huo. Kwa upande wa
Tanzania, Kamishna Msaidizi wa Maendeleo ya Nishati kutoka Wizara ya
Nishati James Andilile amemwakilisha Katibu Mkuu Wizara hiyo.
Waziri wa Nishati Dkt. Medard
Kalemani akizungumza jambo wakati wa mkutano huo. Wanaomsikiliza ni
ujumbe wa Tanzania ulioshiriki Mkutano huo.
Sehemu ya Washiriki wa Mkutano huo kutoka nchi mbalimbali za Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Waziri wa Nishati Dkt. Medard
Kalemani akisalimiana na Wataalam mbalimbali kutoka Wizara ya Nishati na
Taasisi mbalimbali zinazohusika na Masuala ya Nishati na Zanzibar baada
ya kukamilika kwa mkutano.
Waziri wa Nishati Dkt. Medard
Kalemani (wa kwanza kulia) akiwa na Wataalam mbalimbali kutoka Wizara
ya Nishati na Kampuni ya Uendelezaji Jotoardhi Tanzania (TGDC) mara
baada ya kuhitimishwa kwa Mkutano wa 12 wa Baraza la Kisekta la
Nishati la Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Mbele, washiriki kutoka nchi ya Rwanda wakiwa katika Mkutano huo.
Waziri wa Nishati wa Tanzani,
Dkt. Medard Kalemani (kulia) na Waziri wa Nchi anayeshughulikia
Nishati kutoka nchini Uganda Dkt. Simon Du’ Ujanga wakitia saini
ripoti ya mkutano huo.
………………………………………………………………………………..
Mkutano wa 12 wa Baraza la
Kisekta la Nishati la Jumuiya ya Afrika Mashariki ulioanza tarehe 30
Oktoba, 2017 Makao Makuu ya Jumuiya hiyo Jijini Arusha, umehitimishwa
leo na Kikao cha Mawaziri wa nchi Wanachama.
Kikao cha Mawaziri kilitanguliwa
na Vikao vya Wataalam wa Sekta ya Nishati , Kikao cha Kamati ya
Nishati ya Baraza hilo na Kikao cha Makatibu Wakuu wa nchi husika.
Katika kikao cha Mawaziri,
viongozi hao pia...
wametia saini ripoti iliyojadiliwa katika vikao hivyo
ambapo masuala kadhaa yakiwemo ya miradi ya Umeme ya mipakani, miradi ya
umeme ya nchi na nchi, Mafuta, Gesi , Nishati Jadidifu , Sera ya
Usalama wa Nishati ya Jumuiya ya Afrika Mashariki pamoja na mambo
mengine yalijadiliwa.
Awali, kabla ya Mawaziri wa nchi wanachama kutia saini ripoti hiyo, pia ilisainiwa na Makatibu Wakuu wa nchi wanachama.
Akizungumza katika mkutano huo,
Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki upande wa Sekta za
Kijamii na Uzalishaji, Christophe Bazivamo ameeleza umuhimu wa kikao
cha Mawaziri na kueleza kuwa, ndiyo kikao ambacho kinatoa mwelekeo wa
utekelezaji wa yale yanayokubaliwa na nchi wanachama. Aidha, Bazivamo
ameendelea kusisitiza kuhusu umuhimu wa nishati kwa ajili ya maendeleo
ya nchi jumuiya ya Afrika Mashariki.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa
Mkutano huo ambaye ni Waziri wa Nchi anayeshughulikia Nishati kutoka
nchini Uganda, Dkt. Simon D’ Ujanga, amesema kuwa, Viongozi wa nchi
zote za Jumuiya hiyo wanayo nia ya kuhakikisha kwamba miradi
iliyokubaliwa na jumuiya inatekelezwa, Pia amewataka nchi wanachama
Kwa upande wake, Waziri wa
Nishati, Dkt. Medard Kalemani amewashukuru wataalam wote ambao
wamefanikisha kukamilika kwa ripoti ambayo itawezesha makubalino
yaliyofikiwa kutekelezwa na jumuiya hiyo na kuongeza kuwa, yote
yaliyojadiliwa katika mkutano huo yanagusa nchi zote na hivyo yanapaswa
kuchukuliwa kwa uzito.
Nchi zilizoshiriki mkutano huo
ni Tanzania, Uganda, Kenya, Rwanda na Burundi. Aidha, Mwenyekiti wa
mkutano huo ilikuwa nchi ya Uganda na Katibu nchi ya Rwanda.
Tanzania katika mkutano husika
imewakilishwa na Wataalam kutoka Wizara ya Nishati, Wizara ya Mambo ya
Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Wizara ya Ardhi Nyumba na
Maendeleo ya Makazi, Wizara ya Maji, Mazingira na Nishati ya Zanzibar,
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Wakala wa Nishati Vijijini (REA),
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) na Wakala wa
Udhibiti wa Shughuli za Mkondo wa Juu wa Mafuta , Zanzibar (ZURA).
No comments :
Post a Comment