Waziri Mkuu Kassim Majaliwa
akizindua kitabu cha Muongozo wa Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini
,katikati ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI .Simba Chawene
,kulia kwake ni Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala Barabara Vijini na Mijini
Mhandisi Victor Seif .Uzinduzi huo umefanyika leo July 2, 2017 katika
ukumbi wa mikutano Chuo cha Mipango Mkoani Dodoma
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.
kulia akimkabidhi kitabu cha Muongozo wa Wakala wa Barabara Vijijini
na Mijini , Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala Barabara Vijini na Mijini
Mhandisi Victor Seif, katikati ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais
TAMISEMI .Simba Chawene . Uzinduzi huo umefanyika leo July 2, 2017
katika ukumbi wa mikutano Chuo cha Mipango Mkoani Dodoma
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa
akihutubia Viongozi wa Mikoa yote Nchini walio hudhuria Uzinduzi wa
Wakala wa Barabara Vijini na Mijini leo july 2,2017, katika ukumbi wa
mikutano Chuo cha Mipango Mkoani Dodoma.
Wakuu wa Mikoa na viongozi mbalimbali wakishuhudia Uzinduzi wa Wawakala wa Barabara Vijijni na Mijini
Picha na ofisi ya Waziri Mkuu
…………………………………………………………….
*Azindua Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini
*Asema utashusha bei ya vyakula mijini
CHANGAMOTO ya usafiri nchini,
hususan maeneo ya vijijini kuwa historia baada ya Waziri Mkuu Kassim
Majaliwa kuzindua Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA).
Amesema wakala huo utasaidia
kuimarisha mtandao wa barabara za vijijini na kuwawezesha wananchi wengi
kusafiri na kusafirisha bidhaa zao kwa urahisi, hivyo kukuza uchumi.
Waziri Mkuu ameyasema hayo leo
(Jumapili, Julai 02, 2017) wakati akizindua wakala huo katika ukumbi wa
Chuo cha Mipango, mjini Dodoma.
“Wakala huu tunaouzindua leo
utakuwa na manufaa makubwa kwa ustawi wa nchi yetu kwa kuongeza chachu
ya uzalishaji mali mashambani kutokana na urahisi wa kufika sokoni,”
“Utashusha bei ya vyakula mijini
na bidhaa za viwandani vijijini kutokana na gharama za usafirishaji wa
mazao kutoka mashambani na bidhaa za viwandani kutoka mijini kupungua,”
Aidha, Waziri Mkuu amesema
manufaa mengine ya wakala huo ni kuboresha na kubadili hali za kimaisha
na kiuchumi kwa wananchi kwani watakuwa wanasafiri kwa muda mfupi.
Pia utawezesha maeneo mengi ya nchi kufikika kwa urahisi, hivyo kuboresha utoaji wa huduma za kijamii kwa wakati.
Katika hatua nyingine, Waziri
Mkuu amesema Mamlaka za Serikali za Mitaa zinakabiliwa na changamoto
mbalimbali katika ujenzi, ukarabati na utengenezaji wa miundombinu ya
barabara ikiwemo ya rushwa katika utoaji wa zabuni.
Amesema jambo hilo halikubaliki
hivyo, amewataka watendaji wa TARURA wahakikishe wanatokomeza vitendo
vya rushwa vilivyokithiri kwenye utoaji wa zabuni, zitolewe kwa watu
wenye uwezo wa kufanyakazi.
Waziri Mkuu amesema changamoto
nyingine ni usimamizi hafifu wa mikataba ya ujenzi, ambapo ameelekeza
isimamiwe vizuri na iwe ya wazi na yenye kutekelezeka.
Akizungumzia vitendo vya baadhi
ya viongozi wa Halmashauri kubadilisha matumizi fedha za barabara,
ameagiza fedha zote zinazotengwa kwa ajili ya miradi ya barabara
zitumike kama ilivyopangwa.
Awali, Waziri wa Nchi Ofisi ya
Rais-TAMISEMI, Mheshimiwa George Simbachawene alisema TARURA ni muhimu
kwa kuwa zinagusa wananchi moja kwa moja na ni kichocheo kikubwa cha
uchumi wa wananchi, hivyo kuinua uchumi wa Taifa wenye msingi imara.
“Barabara hizi zinachochea
kilimo katika ngazi ya jamii, zinaboresha ufikaji kwenye huduma za
kijamii kama afya, elimu, maji na masoko, hivyo kuliwezesha Taifa kuwa
na jamii imara kiafya, kiakili na kiuchumi,”.
Kutokana na umuhimu wa mtandao
wa barabara za Vijijini na Mijini, Mheshimiwa Simbachawene ameomba
mgawanyo wa mapato ya Mfuko wa Barabara wa asilimia 70 kwa TANROADS na
asilimia 30 kwa Halmashauri uangaliwe upya, ambapo Waziri Mkuu
ameridhia.
Waziri Mkuu alisema “Naamini kwa
kuanzishwa TARURA sasa hoja hii inajadilika, tumieni taratibu zilizopo
ili maamuzi yaweze kufanyika,”.
Mtandao wa barabara za Mamlaka ya Serikali za Mitaa ni kilomita 108,942.2 ambao ni Zaidi ya nusu ya barabara za Kitaifa.
No comments :
Post a Comment