Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akikabidhi ngao ya ushindi wa kwanza Bw. James Mlowe Meneja Masoko na Uhusiano wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF huku akiwa na furaha baada ya shirika hilo kupata ushindi wa kwanza kwa makampuni ya Mifuko ya Hifadhi ya Jamii pamoja na Bima
wakati wa ufunguzi rasmi wa maonyesho ya Sabasaba yanayoandaliwa na
Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara ya Nje (TANTRADE) yanayoendelea
kwenye viwanja vya Sabasaba Barabara ya Kilwa jijini Dar es salaam kila
mwaka kuanzia tarehe 1 mwezi Julai, Kutoka kulia wanaoshuhudia ni Mwenyekiti wa Bodi ya (TANTRADE) Bw. Christopher Chiza na Waziri wa Viwanda , Biashara na Uwekezaji, Mh.Charles Mwijage.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akifurahia jambo mara baada ya
kumkabidhi ngao ya ushindi wa kwanza kwa Meneja wa Masoko na Uhusiano wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF Bw. James Mlowe baada ya kupata ushindi wa kwanza kwa kipengele cha Mifuko ya Jamii pamoja na Bima
katika ufunguzi rasmi wa maonyesho ya Sabasaba yanayoandaliwa na
Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara ya Nje TANTRADE yanayoendelea kwenye
viwanja vya Sabasaba Barabara ya Kilwa jijini Dar es salaam kila mwaka
kuanzia tarehe 1 mwezi Julai, Kutoka kulia wanaoshuhudia ni Mwenyekiti wa Bodi ya (TANTRADE) Bw. Christopher Chiza na Waziri wa Viwanda , Biashara na Uwekezaji, Mh.Charles Mwijage.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akizungumza wakati wa uzinduzi wa maonyesho hayo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akitembelea
mabanda mbalimbali mara baada ya kukabidhi tuzo kwa washindi wa
maonyesho hayo wakati alipoyazindua rasmi siku ya jumamosi iliyopita.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono wananchi mbalimbali waliojitokeza katika maonyesho hayo wakati wa uzinduzi siku ya jumamosi iliyopita.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akiondoka
kwenye viwanja vya Sabasaba mara baada ya kukabidhi tuzo kwa washindi
na kuyafungua rasmi maonyesho hayo siku ya jumamosi iliyopita.
No comments :
Post a Comment