Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema
Nchimbi (katikati) akisikiliza kwa maelezo ya tathmini ya athari za
mazingira na kijamii kwa mradi wa bomba la mafuta, wa kwanza kulia kwake
ni Katibu Tawala Mkoa Dkt Angelina Lutambi na kushoto ni Mtathmini wa
mazingira Bi Saada Juma kutoka kampuni ya JSB.
Ramani inayoonyesha maeneo ya
wilaya tatuza Mkoa wa Singida ambapo tathmini ya athari za mazingira na
kijamii kwa mradi wa bomba la mafuta litakalopita kutoka Uganda hadi
Tanga.
Wadau wa sekta mbalimbali zinazohusika
na mazingira kutoka mkoa wa Singida wakifuatilia kwa umakini maelezo ya
tathmini ya athari za mazingira na jamii kwa ujenzi wa bomba la mafuta litakalopita kutoka Uganda hadi Tanga.
Mtaalamu Bw. Lalit Kumar kutoka kampuni ya RSK itakayohusika na ujenzi wa bomba la mafuta litakalopita kutoka Uganda hadi Tanga.
…………………………………………………………………………….
Wananchi wa Wilaya tatu za
Makalama, Iramba na Singida Mkoani Singida ambazo bomba la mafuta kutoka
Uganda hadi Tanga linapita wanapaswa kutoka ushirikiano wa kutosha
katika
hatua zote za ujenzi wa bomba hilo ili wanufaike na fursa
zitakazopatikana kwa uwepo wa mradi huo.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt.
Rehema Nchimbi ametoa rai hiyo katika kikao cha tathmini ya athari za
mazingira na za kijamii katika mradi wa bomba la mafuta ambapo
watathmini watapita maeneo yote ambapo bomba hilo litapita ili kupata
maoni yao ili yaweze kuzingatiwa wakati wa utekelezaji wa mradi huo.
Dkt. Nchimbi amesema wananchi
wanapaswa kuwajulisha watathmini hao kila kitu kuhusu hali ya mazingira
na kijamii ili mradi huo usiharibu mazingira au upunguze baadhi ya
athari wakati wakujenga bomba hilo.
Ameongeza kuwa wananchi wasiwe na
wasiwasi kuhusu fidia kwa maeneo ambapo bomba litapita kwakuwa
watalipwa vizuri fidia zao na hivyo wanapaswa kuruhusu mradi huo upite
katika maeneo yao bila wasiwasi na pia wasianze kuendeleza maeneo ambayo
wamesikia mradi utapita kwa kigezo tu cha kupata fidia kubwa.
Kwa upande wake Mtathmini wa
Mazingira Saada Juma kutoka kampuni ya JSB ambayo inafanya tahmini hiyo
amesema wanatekeleza matakwa ya kisheria katika kufanya tahmini hiyo na
wataifanya kwa kasi kubwa ili ujenzi rasmi wa mradi uwahi kufanyika.
Saada amesema mradi huo utakua
kambi mbalimbali na kwa mkoa wa Singida kambi itakuwa katika kata ya
Msisi ambapo uwepo wa kambi hiyo utaongeza uchumi wa kata na wilaya
hiyo.
Amesema vijana wa Singida
wajiandae kwa ajili ya kupata ajira mbalimali katika mradi huo, baadhi
ya miundombinu itaboreshwa pamoja na uchumi kukukua kwa kuuza bidhaa na
kutoa huduma kwa watakaokuwa wakiishi katika kambi hiyo.
Tathmini ya athari za mazingira
na za kijamii kwa wilaya za Singida, Mkalama na Iramba ambapo mradi wa
bomba la mafuta kutoka Uganda mpaka Tanga itaana mapema wiki ijayo.
No comments :
Post a Comment