Thursday, May 4, 2017

UTARATIBU MPYA WA UWASILISHAJI WA MICHANGO NA MALIPO MENGINEYO KWA WAAJIRI NA WANACHAMA WA MFUKO WA TAIFA WA BIMA YA AFYA (NHIF)

index
Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) umefanya maboresho ya uimarishaji wa mfumo wa uwasilishaji wa michango na malipo ya huduma nyinginezo kutoka kwa waajiri na wanachama wake kupitia benki.
Kutokana na maboresho hayo, kuanzia tarehe 1 Juni 2017, mwajiri au mwanachama anatakiwa kuwa na namba rejea ya malipo (payment reference number) kila anapowasilisha
michango au kufanya malipo kupitia tawi lolote la benki ya NMB.
Ili kupata namba rejea ya malipo, waajiri na wanachama wanatakiwa kutekeleza utaratibu ufuatao:
  • Mwajiri anatakiwa kutumia mfumo wa mtandao unaopatikana kupitia anuani https://verification.nhif.or.tz/serviceportal na kufuata maelekezo hatua kwa hatua. Maelekezo kamili ya namna ya kutumia mfumo huo yanaweza kupakuliwa kwa kubonyeza eneo lililoandikwa “Download”;
  • Pamoja na mfumo huo, mwanachama anaweza pia kutumia simu ya mkononi kwa kupiga namba *152*00# na kufuata maelekezo. Huduma hii inapatikana kupitia mitandao ya Airtel, Vodacom, Tigo na Zantel tu.
  • Nukuu namba rejea ya malipo na kuitumia wakati wa kufanya malipo halisi (actual payment) kwenye benki ya NMB kupitia njia zake mbalimbali za ukusanyaji fedha (cash collection channels) ikiwemo njia ya simu za mkononi (mobile payment), kaunta za matawi ya benki hiyo n.k.
Kwa msaada zaidi tafadhali wasiliana na kituo cha huduma kwa wateja kwa kupiga simu namba 0800 110063 (bila malipo)
Imetolewa na;
KAIMU MKURUGENZI MKUU
Mei 2, 2017

No comments :

Post a Comment