Thursday, May 4, 2017

Ufinyu Wa Bajeti Ni Kikwazo Kwa Huduma Za Uzazi Wa Mpango

8
 Ufinyu
wa bajeti kwa ajili ya huduma za uzazi wa mpango imekuwa ndicho kikwazo
kikuu katika kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi hapa nchini ambapo
katika miaka sita iliyopita kiwango cha juu sana kilichotengwa na
kutolewa kwa mwaka ni shilingi bilioni tano tu.
Hayo yameelezwa
na Dkt. Faustine Ndugulile, ambaye ni Mjumbe wa Chama cha Wabunge kuhusu
Idadi ya Watu na Maendeleo mwishoni mwa wiki wakati akiongea jijini Dar
es Salaam kuhusu changamoto cha uzazi wa mpango hapa nchini Tanzania.
Dkt
Ndugulile alisema kuwa huduma za uzazi wa mpango zinahitaji shilingi
bilioni 20 kila mwaka lakini kati ya mwaka 2010/11 na 2015/16 ni bilioni
5 tu zilizotengwa na kutolewa kila mwaka zilikuwa pungufu sana
ukilinganisha na mahitaji halisi. Kiwango cha juu kwa mwaka kilikuwa ni
kiasi cha shilingi bilioni tano tu ambazo zilitengwa na kutolewa, sawa
na asilimia 25 tu ya mahitaji yote kwa mwaka husika.
‘Tafiti
zinaonyesha kuwa Tanzania ni moja kati nchi zenye vifo vingi vitokanao
na uzazi duniani, ambapo vifo 556 hutokea kwa kila vizazi hai 100,000;
ikimaanisha kuwa zaidi ya akinamama 50 hufariki kila siku kutokana na
matatizo ya uzazi’, alisema Ndungulile.
Dkt Ndugulile aliongeza
kuwa zaidi ya watoto 100,000 hufariki kabla ya kutimiza miaka mitano,
kati ya hao zaidi ya 50,000 hufariki kabla ya kuzaliwa na nusu yao
wakati wa kuzaliwa, huku wenzao wapatao 40,000 wakifariki dunia kwenye
siku 28 za mwanzo baada ya kuzaliwa. Licha ya ufinyu wa bajeti, Vifo
vingi vya uzazi hutokea kwa sababu wanawake wanakosa kufikia huduma
ambazo wanazihitaji ikiwemo uzazi wa mpango.
Sababu zingine ni
kubeba mimba wakati wa umri mdogo, kutoa mimba kwa njia zisizo salama,
kuendelea kubeba mimba wakiwa na umri mkubwa ambao ni zaidi ya miaka 35,
na kukosa ufahamu wa jinsi ya kutoa nafasi baada ya kujingua ili kubeba
mimba inayofuata.
Mpango wa Taifa Uliokasimiwa wa Uzazi wa
Mpango (NFPCIP) uliweka lengo la kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi
kupitia kuongeza matumizi ya uzazi wa mpango hadi kufikia asilimia 60 ya
wanawake walio katika umri wa uzazi ilipofika mwaka 2015. Ni asilimia
32 tu ya wanawake walifikiwa. Lengo hilo limehishwa kwa ajili ya
kufikiwa mwaka 2020.
Akisisitiza kuhusu umuhimu wa za uzazi hapa
nchini, Dr. Faustine Ndungulile alisema kuwa “ufinyu wa bajeti umekuwa
ikiwanyima wanawake wenye umri mdogo huduma za uzazi wa mpango ambazo ni
muhimu kwa afya zao, watoto wao, na maendeleo yao na taifa. Wanawake
wanaoanza uzazi katika umri mdogo na kuzaa kwa mfululizo wanakosa fursa
za kujiendeleza kielimu, kiuchumi, na kijamii; na kuwafanya wasiweze
kufikia upeo wa ndoto zao za kimaendeleo, hali ambayo pia huwapata
watoto wao.”

No comments :

Post a Comment