Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikaribishwa na Waziri wa
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa katika moja ya
banda lililopo katika ukumbi wa Kimataifa wa mikutano wa Kikwete kabla
ya kufungua Mkutano wa 20 wa Mashauriano ya Bodi ya Makandarasi (CRB),
uliofanyika mjini Dodoma.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (kulia), akikabidhiwa
zawadi na mmoja wa wafanyakazi wa Kampuni ya Denim Eleveators (kushoto)
baada ya kukagua banda hilo katika ufunguzi wa Mkutano wa 20 wa
Mashauriano ya Bodi ya Makandarasi (CRB), uliofanyika mjini Dodoma.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan na Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa wakiwa katika ufunguzi wa
Mkutano wa 20 wa Mashauriano ya Bodi ya Makandarasi (CRB), uliofanyika
mjini Dodoma.
Msajili wa Bodi ya Makandarasi
Eng. Reuben Nkori akitoa taarifa ya kiutendaji kwa Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan wakati wa
ufunguzi wa Mkutano wa 20 wa Mashauriano ya Bodi ya Makandarasi (CRB),
uliofanyika mjini Dodoma.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akizungumza na Makandarasi
waliohudhuria Mkutano wa Mashauriano ya Bodi ya Makandarasi (CRB),
wenye kauli mbiu “Miaka 20 ya CRB Utendaji wa Makandarasi unaozingatia maadili na sheria kama mkakati wa kuaminiwa na waajiri”, uliofanyika mjini Dodoma.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia Makandarasi
waliohudhuria Mkutano wa Mashauriano ya Bodi ya Makandarasi (CRB), wenye
kauli mbiu “Miaka 20 ya CRB Utendaji wa Makandarasi unaozingatia maadili na sheria kama mkakati wa kuaminiwa na waajiri”, uliofanyika mjini Dodoma.
Makandarasi wakisikiliza hotuba ya
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Mashauriano ya Bodi ya
Makandarasi (CRB), wenye kauli mbiu “Miaka 20 ya CRB Utendaji wa Makandarasi unaozingatia maadili na sheria kama mkakati wa kuaminiwa na waajiri”, uliofanyika mjini Dodoma.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (kulia), akiteta jambo na Mkuu wa
Mkoa wa Dodoma Mhe. Jordan Rugimbana (kushoto), wakati wa ufunguzi wa
Mkutano wa 20 wa Mashauriano ya Bodi ya Makandarasi (CRB), uliofanyika
mjini Dodoma.
Mwakilishi kutoka Wakala wa
Barabara Nchini (TANROADS), akipokea tuzo kutoka kwa Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan wakati wa
ufunguzi wa Mkutano wa 20 wa Mashauriano ya Bodi ya Makandarasi (CRB),
uliofanyika mjini Dodoma.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya
pamoja na Watendaji wa Bodi ya Usajili ya Makandarasi (CRB), na viongozi
wengine wa Wizara katika ufunguzi wa Mkutano wa 20 wa mwaka wa CRB,
uliofanyika mjini Dodoma.
………………………….
Serikali imewataka Makandarasi
kuwajibika na kufanya kazi zao kwa ufanisi na weledi ili kuishawishi
Serikali kuwaamini na kuwapatia zabuni za kutekeleza miradi mikubwa
nchini.
Akizungumza katika ufunguzi wa
Mkutano wa 20 wa Mashauriano ya ...
Bodi ya Makandarasi (CRB), mjini Dodoma,
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu
Hassan, amesema kuwa miradi mingi mikubwa nchini imekuwa ikitekelezwa na
Makandarasi kutoka nje ya nchi hali inayopelekea Serikali kutumia fedha
nyingi kuwalipa Makandarasi hao.
“Muda umefika sasa kwa makandarasi
wazawa kuungana na kuomba zabuni za kutekeleza miradi mikubwa
itakayowajengea uwezo kama ujenzi wa bomba la Mafuta kutoka Uganda hadi
Tanga, Reli ya Kisasa na miradi mingine”, amesema Makamu wa Rais.
Aidha, amefafanua kuwa kutekelezwa
kwa miradi hiyo na Makandarasi wazawa kutaokoa fedha za ndani za
watanzania na hivyo kupelekea fedha hizo kubaki nchini na vijana kupata
ajira.
Sambamba na hilo Makamu wa Rais
amewasisitiza Makandarasi hao kuwa wa kwanza kuomba zabuni pindi
zinapotangazwa kwani Serikali ya Awamu ya Tano itatoa kipaumbele kwa
Makandarasi wazawa wote nchini.
Makamu wa Rais ameitaka CRB
kuhakikisha inasimamia Makandarasi hao kutekeleza miradi kwa muda
uliopangwa pamoja na kufuata maadili katika utendaji wao wa kazi.
Kuhusu suala la ulipaji wa madeni
ya Makandarasi Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema kuwa kwa sasa Serikali
inendelea kufanya uhakiki wa madeni hayo ambapo zoezi la malipo litaanza
mara baada ya uhakiki huo kukamilika.
Kwa Upande wake, Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa amesema kuwa kutokana
na umuhimu wa kuwathamini Makandarasi wazawa Wizara imetenga miradi
maalum kwa ajili ya kuwajengea uwezo Makandarasi hao.
Profesa Mbarawa amewahakikishia
makandarasi hao kupata fursa kwa zabuni zinazotangazwa na Wizara kwa
kila Mkandarasi mwenye sifa atakayeomba zabuni hizo.
“Makandarasi msisite kuomba zabuni
pindi zinapotangazwa, naahidi nitasimamia kwa uaminifu na kuhakikisha
kila mkandarasi mwenye sifa anapata zabuni kwa mujibu wa sheria”,
amesema Profesa Mbarawa.
Naye, Mwenyekiti wa Bodi ya
Usajili wa Makandarasi nchini, Eng. Consolata Ngimbwa amemhakikishia
Makamu wa Rais kuwa watatumia mkutano huo kujadili changamoto
zinazowakabili na hivyo kuja na mapendekezo sahihi ya kutatua changemoto
hizo.
Mkutano huo wa siku mbili wenye kauli mbiu isemayo “Miaka 20 ya CRB, utendaji wa Makandarasi unaozingatia maadili na Sheria kama mkakati wa kuaminiwa na waajiri” una
lengo la kuwakutanisha makandarasi wa ndani na nje ya nchi kwa lengo
la kujadili kwa pamoja changamoto zao na kuzitafutia ufumbuzi.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uhukuzi na Mawasiliano.
No comments :
Post a Comment