Monday, May 1, 2017

PPF WAUNGANA NA WENZAO KUADHIMISHA SIKU YA WAFANYAKAZI DUNIANI

NA K-VSI BLOG/Khalfan Said

WAFANYAKAZI
 wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, wameungana na wenzao jijini Dar es salaam
 kuadhimisha siku ya wafanyakazi Duniani maarufu kama Mei Mosi.
Kitaifa
sherehe hizo zinaongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John
Pombe Magufuli mjini Moshi ambapo kauli mbiu ya mwaka huu ni “Uchumi wa Viwanda
uzingatie Haki, Maslahi na Heshima ya wafanyakazi.”
Aidha
jijini Dar es Salaam, Wafanyakazi wa PPF na wengine kutoka sekta ya Umma na
Binafsi, walifanya matembezi kutoka eneo la Mnazi Mmoja hadi uwanja wa Uhuru
huku wakiongiozwa na brass band ya Jeshi la Magereza.
Kwa upande
wao wafanyakazi wa PPF  walianza kwa
kukusanyika kwenye ofisi za Makao Makuu ya Mfuko huo barabara ya
Samora/Morogoro ambapo walipewa maelekezo ya umuhimu wa ushiriki wao katika maetembezi
hayo na kujiunga na wenzao eneo la kuanzia matembezi pale Mnazi moja.
Mgeni
rasmi katika sherehe za Mei Mosi jijini Dar es Salaam, alikuwa Mkuu wa Wilaya
ya Temeka, Bw.
Felix Lyaviva, ambaye alipokea maandamano ya
wafanyakazi na magari kadhaa kutoka taasisi za umma na binafsi yakionyesha
huduma zitolewazo na taasisi hizo.
Huduma
zitolewazo na PPF ni pamoja na kulipa Mafao ya Uzeeni, Mafao ya
Wategemezi,Mafao ya Elimu, Mafao ya Kiinya Mgongo, Mafao ya Kifo, Mafao ya
Ugonjwa na Mafao ya Uzazi. Lakini pia kazi nyingine za Mfuko huo ni kusajili
wanachama kupitia mfumo wa uchangiaji wa hiari ujulikanao kama “Wote Scheme”

Baadhi ya wafanyakazi wa PPF, wakiwa kwenye matembezi ya kuadhimisha Mei Mosi jijini Dar es Salaam Leo.

Kiongozi wa kundi la wafanyakazi WA PPF, walioshiriki matembezi ya kuadhimisha siku ya wafanyakazi duniani, Mohammed Siaga, (kushoto), akizungumza muda mfupi kabla ya kuanza matembezi hayo.







No comments :

Post a Comment