Monday, May 1, 2017

MKURUGENZI MKUU WA WCF MASHA MSHOMBA AWAHAMASISHA WAAJIRI KUJISAJILI NA MFUKO HUO, WAUNGANA NA WENZAO KUADHIMISHA MEI MOSI, MOSHI NA DAR ES SALAAM




Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (Workers Compesation Fund – WCF), Masha Mshomba, (pichani) amewahamasisha waajiri nchini kujisajili katika mfuko huo kwani mkombozi mkubwa kwa waajiri na wafanyakazi.

Mshomba
ametoa rai hiyo leo wakati wa siku ya wafanyakazi duniani ‘Mei Mosi”
iliyofanyika kitaifa katika viwanja vya Ushirika Moshi mkoani
Kilimanjaro ambapo mgeni rasmi katika sherehe za Mei Mosi mwaka huu
alikuwa rais John Pombe Magufuli. 

Mfuko
wa Fidia ni mkombozi kwa waajiri na wafanyakazi nchini kwa sababu
umekuja katika kipindi ambacho huko nyuma tulikuwa hatuna chombo
hiki,wafanyakazi walikuwa wakipata ajali na magonjwa yanayotokana na
kazi bila kupata fidia sasa mfuko umekuja mambo hayo yatakuwa historia. 

Mshomba
alisema  WCF ni faraja kwa waajiri kwani utawawezesha kujikita katika
uzalishaji tu, na WCF kubaki na jukumu la kumuhudumia mfanyakazi
anapoumia, au kuugua. Alsema Mshomba. Alisema pamoja na kwamba waajiri
ndiyo wachangiaji wakuu,mfuko wa WCF umewaondolea mzigo wa kuhangaika na
mtumishi pale anapopata ajali, au maradhi yatokanayo na kazi
anazofanya.

“Tunawasihi
sana waajiri waendelee kujisajili katika mfuko wa WCF kwa haraka kabisa
ili waweze kunufaika wao na wafanyakazi wao,mfanyakazi akipata ajali
atapata huduma ya matibabu na kama amepata ulemavu basi atapata fidia
katika malipo ya pensheni ya kila mwezi”,aliongeza Mshomba. 

Katika
kusherehekea sherehe za Mei Mosi mwaka 2017 mfuko wa WCF umetoa elimu
kwa wafanyakazi na wananchi mbalimbali waliofika katika banda lao lakini
pia wafanyakazi wa WCF wameshiriki katika maandamano ya wafanyakazi
kutoka sekta mbalimbali za umma na binafsi katika viwanja vya Ushirika
Moshi. Kutoka Dar es Salaam, Khalfan Said wa K-VIS BLOG anaripoti kuwa

Wfanyakazi
wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), wameungana na wenzao jijini Dar es
salaam kuadhimisha siku ya wafanyakazi Duniani maarufu kama Mei Mosi kwa
matembezi kutoka Mnazi Mmoja hadi uwanja wa Uhuru.
Kitaifa sherehe
hizo zimeongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe
Magufuli mjini Moshi ambapo kauli mbiu ya mwaka huu ni “Uchumi wa Viwanda
uzingatie Haki, Maslahi na Heshima ya wafanyakazi.”
Mgeni
rasmi katika sherehe za Mei Mosi jijini Dar es Salaam, alikuwa Mkuu wa Wilaya
ya Temeka, Bw.

Felix Lyaviva, ambaye alipokea maandamano ya wafanyakazi na magari kadhaa
kutoka taasisi za umma na binafsi yakionyesha huduma zitolewazo na taasisi
hizo.
WCF
ni Mfuko ulioanzishwa kwa sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi namba 20 ya mwaka
2008 na ndio Mfuko unaowajibika kutoa Mafao ya Fidia kwa Wafanyakazi walioumia,
au kupatwa na maradhi yaliyoababishwa na kazi wanazozifanya lakini pia kutoa
Fidia kwa wategemezi pindi Mfanyakazi anapofariki kwa kuzingatia vigezo
vilivyowekwa.
Wafanyakazi wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (Workers Compesation Fund – WCF)  wakiwa katika maandamano
Rais John Pombe Magufuli akipokea maandamano ya wafanyakazi wakati wa maadhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani ‘Mei Mosi’ mwaka 2017 katika viwanja vya Ushirika Moshi mkoani Kilimanjaro
Wafanyakazi kutoka Mfuko wa WCF wakiwa katika banda la WCF wakati wa maadhimisho ya sherehe za Mei Mosi mwaka 2017 ambapo wananchi walipata fursa ya kupata elimu kuhusu mfuko huo
Wananchi wakiwa katika banda la WCF
Wananchi wakiwa katika banda la WCF wakipata maelezo kutoka kwa wafanyakazi wa mfuko huo
Wafanyakazi wa mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi -WCF wakibadilishana mawazo baada ya sherehe za Mei Mosi kumalizika katika viwanja vya Ushirika Moshi mkoani Moshi.Kushoto ni Mkurugenzi wa Huduma za Matibabu na Tathmini WCF, Dkt. Abdulssalaam Omary,katikati ni Rajabu Ruje,kulia ni Afisa Uhusiano WCF, Zaria Mmanga.
Picha zote na Kadama Malunde- Malunde1 blog
 Baadhi ya wafanyaakzi wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), wakiungana na wenzao katika maandamano ya kuadhimisha siku ya Wafanyakazi Duniani ambapo kiraifa yamefanyika kwenya uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.










No comments :

Post a Comment