Friday, May 5, 2017

MGOMBEA URAIS UFARANSA ARUSHIWA MAYAI NA WAANDAMANAJI


NA K-VIS BLOG/Mashirika ya Habari
MGOMBE urais wa Ufaranasa, mwanamama Marine Le Pen,(48), amerushiwa mayai na waandamanaji dakika chache kabla ya kuongea na waandishi wa habari.
Walinzi wake walilazimika kumuondoa kwa haraka huku wakimfunika baada ya mayai kuvurumishwa na waandamanaji hao wanaopinga sera za mgombea huyo ambaye hataki wahamiaji.
Tukio hilo lililotokea Mei 4, 2017, limekuja siku moja baada ya kushiriki katikammdahalo wa TV na mpinzani wake, Emmanuel Marcon.
Hata hivyo hakuna yai lililompata, baada ya walinzi wake kujenga “ukuta” na kumuondosha kwa haraka kwenye eneo la tukio.
Kiasi cha waandamanaji wapatao 50, walikuwa wamejipanga, wakati Mama Le Pen alipowasili kwenye kampuni ya usafirishaji kwenye mji wa Magharibi wa Dol-de-Bretagne na kuanza kubuirumisha mayao huku wakipiga kelele za fashist.

 Bibi Le Pen akiwasili eneo alikorushiwa mayai
 Waandamanaji wanaopinga sera za Bbi Le Pen
 Walinzi wa Bibi Lepen, "wakijenga ukuta" kumuokoa na "makombora" ya mayai
 Bi Le Pen akisindikizwa na walinzi wake
Emmanuel Marcon

No comments :

Post a Comment