Lakini katika soko hili ambalo ili uaminike na kujulikana ndipo ufanye
vizuri, wamiliki wa biashara hawana budi kutafakari kwa makini kushiriki
kwenye maonyesho mbalimbali. Jumia Travel ingependa kukuelimisha kuwa
ukizingatia yafuatayo basi biashara yako itanufaika vya kutosha:Weka malengo yatakayoisaidia biashara yako.
Usikurupuke kushiriki kwenye
maonyesho yoyote kama hujajua malengo ya kufanya hivyo. Hakikisha
unaweka malengo ya kimauzo kwa wafanyakazi wako kabla ya kushiriki;
hakikisha unajenga ukaribu na washiriki wote kwenye maonyesho kwani
wanawezakuja kuwa wateja wako siku za usoni na mwisho kabisa hifadhi
kumbukumbu ya watu unaowasiliana nao ili uje kufuatilia maendeleo yao
baadae.
Jifunze kipi kinafaa na kipi hakifai. Katika kushiriki kwenye maonyesho
ya namna hii sio siku zote yatakuwa na mafanikio makubwa. Hivyo basi
hakikisha unachunguza ni mabanda yapi yanawavutia watu wengi zaidi na
ujifunze mbinu zao; hifadhi kumbukumbu za bei na ofa wanazotoa
washindani wako kisha ulinganishe na zako; jifanye kuwa ni mteja, kisha
tazama watoa huduma wengine wanawasiliana kwa namna gani na wewe, na
wanakuwa na malengo yapi ya kibiashara. Lazima kuna vitu utajifunza
tofauti na unavyofanya wewe.
Kuza
na imarisha jina la biashara yako. Zipo mbinu nyingi katika
kulifanikisha hili hususani kama biashara yako ndiyo kwanza inachipukia.
Baadhi yake ni kama vile; jaribu kuweka banda lako mahali ilipo kampuni
kubwa (kama utapata fursa hiyo) ili kukuza muonekano wako kwani wateja
watakapotembelea hapo watavutiwa na kufanya hivyo kwako pia; tengeneza
mabango yenye kuvutia na kuonekana kwa urahisi ili kuwavutia wateja wako
na wale wapya; ni vema kujumuisha taarifa zako za kwenye mitandao ya
kijamii ili wahudhuriaji waweze kujiunga nawe huko.
Jaribu kufanya mauzo ukiwa maonyeshoni. Ingawa linaweza kuwa sio lengo
lako kuu lakini ni lazima kufanya hivyo kwani pia inaweza kukusaidia
kurejesha fedha ulizozitumia. Kama inawezekana, jaribu kufanya mauzo
unapokuwa maonyeshoni wakati wahudhuriaji wakiwa na shauku ya kununua
bidhaa; nenda na bidhaa zako ili kufanya mauzo papo hapo, pindi
wahudhuriaji wanapoonyesha kuvutiwa na bidhaa na huduma zako; endapo
utashindwa kufanya mauzo kwenye maonyesho, chukua mawasiliano ya
wahudhuria na kisha panga kuwasiliana nao siku za usoni.
Hakikisha
unachagua maonyesho sahihi kwa biashara yako. Kabla ya kukata shauri la
kushiriki kwenye onyesho lolote hakikisha kwamba ni sahihi kwa kampuni
yako. Kushiriki kwenye onyesho ambalo hautotimiza malengo yako ni sawa
na kupoteza muda na rasilimali zako ambazo ungeweza kuzielekeza sehemu
nyingine. Je, malengo yako ni kuuza bidhaa au kutoa huduma? Au kujenga
na kuimarisha mahusiano yako ya kibiashara na wadau wengine kwenye
tasnia moja? Haya yote ni muhimu kuyatambua kabla ya kukata shauri na
kushiriki.
Lakini hayo yote yatategemeana na kuchagua maonyesho sahihi/yanayofaa
kwa ajili ya kampuni/biashara yako. Jumia Travel inakushauri kuwa
unaweza kufanya hivyo kwa kuwauliza wenzako au washindani wako.
Kushiriki maonyesho yasiyo sahihi kunaweza kukugharimu vitu vingi zaidi
ya gharama za ushiriki.
No comments :
Post a Comment