Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akinyanyua juu Taarifa na
vitabu vye majina 9,932 ya watumishi wenye vyeti vya kugushi.
Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe na kufungua
boksi kubwa lenye majina ya watumishi zaidi ya 9,932 waliobainika kuwa na vyeti
vya kugushi mara baada ya kupokea Taarifa ya zoezi la uhakiki wa vyeti kwa watumishi wa umma kutoka kwa Waziri wa
Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala bora Angela
Kairuki katika Ukumbi wa Chimwaga mjini Dodoma
Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan,
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa , Waziri wa Elimu Profesa Joyce Ndalichako, Spika
wa Bunge Job Ndugai, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa
Umma na Utawala bora Angela Kairuki wakiminya kitufe kuashiria maadhimisho ya
miaka 10 ya Chuo Kikuu cha Dodoma UDOM katika ukumbi wa Chimwaga mkoani Dodoma.
Makamu wa Rais
Samia Suluhu Hassan akihutubia katika Ukumbi wa Chimwaga.
|
Waziri Mkuu
Kassim Majaliwa akihutubia katika hadhara hiyo katika Chuo kikuu cha Dodoma
UDOM.
Baadhi ya
viongozi mbalimbali wakifatilia kwa makini Hotuba iliyokuwa ikitolewa na Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika maadhimisho
ya miaka 10 ya Chuo cha UDOM toka kuanzishwa kwake.
Baadhi ya
Makatibu wakuu pamoja na viongozi mbalimbali wa Serikali, wanafunzi pamoja na
walimu wa UDOM wakipiga makofi wakati
wakimkaribisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
wakati akiwasili katika ukumbi wa Chimwaga mkoani Dodoma.
Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Taarifa ya miaka 10
ya Chuo kikuu cha Dodoma UDOM kutoka kwa Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa
Idris Kikula, katika ukumbi wa Chimwaga mkoani Dodoma. (PICHA NA IKULU)
No comments :
Post a Comment