Mkuu wa wilaya ya Iringa Mh Richard Kasesela akiwa amembeba mtoto huyo.
Leo
mida ya saa 2 asubuhi katika maeneo ya Stand kuu ya mabasi aliibiwa
mtoto mchanga mweney umri wa miezi 5. Mtoto huyo aliibiwa na binti
ambaye alikuwa amekuja kutafuta kazi.
Akieleza tukio hilo Mama yake Bi Asha Shaban Lauza alisema ” nikiwa
naosha vyombo binti huyu ambaye toka jana alikuwa anatafuta kazi alianza
kumpa maziwa mtoto yaliyo kwenye chupa mpaka mtoto akamaliza , baadae
mtoto akajinyea basi bila wasiwasi nikampa shilingi elfu kumi ili
akanunue pampasi duka la pili tu akanyanyuka na mtoto kwenda dukani toak
asubuhi mpaka sasa usiku hautja muona” .
Mkuu wa wilaya ya Iringa Mh Richard Kasesela alifika eneo la tukio
baada ya kumhoji mzazi akagundua walichelewa kutoa taarifa polisi. Baada
ya msako muda was saa 3 usiku mtoto alipatikana eneo la Mkungugu km 33
kutoka Iringa Mjini.
Binti wa miaka 14 (Jina linahifadhiwa) alikuwa akitoroka na mtot huyo
gari la polisi la doria likishirikiana na wananchi wa kijiji cha
Mkungugu lilifanikiwa kumuweka chini ya ulinzi mwizi huyo wa mtoto. Mkuu
wa Wilaya alifika akiongozana na mama Mzazi wa mtoto pamoja na Diwani
wa kata ya Kisinga Mh Ritha Mlagala.
Binti mwizi yupo kituo cha polisi akiendelea kuhojiwa na mama mzazi
baada ya kuandika maelezo alipewa fomu ya matibabu na kumpeleka mtoto
hospitali.
Mkuu wa wilaya ya Iringa Mh Richard Kasesela amekemea vikali kitendo
cha uzembe wa mama huyu na wazazi kwa ujumla “pamoja na mama huyu kuwa
na uchungu wa mtoto bado ana mashtaka ya kujibu ya uzembe, watu tusio
wajua tusiwape watoto wetu hata kidogo huu ni uzembe wa hali ya juu”
alisisitiza
Mkuu wa wilaya. Pichani anaonekana mtoto Latifa akiwa ambebwa na Mkuu
wa wilaya walipofika kituo cha polisi. Picha zingine ni za eneo la
kijiji cha Mkungugu barabani alipokamatwa binti mwizi akiwa na mtoto
usiku wa saa 3.
No comments :
Post a Comment