Wednesday, February 1, 2017

KUMBE JPM NI MWANA DIPLOMASIA MAHIRI USIPIME


COB7
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Rais wa Misri Abdel Fattah El Sisi mara baada ya kumaliza mazungumzo yao katika moja ya Ofisi za Makao Makuu ya Umoja wa Afrika (AU) mjini Addis Ababa nchini Ethiopia.
…………………………………………………………………..
Na Lugenzi Kabale
KUNA JAMBO muhimu sana nimeliona na nimejifunza katika mwili na akili za JPM leo kutokana na ile mikutano aliyofanya Addis Ababa na Marais wa Egypt, Uganda, AfDB na PM wa Ethiopia nchini Ethiopia.

JAMBO hilo limenithibitishia usemi unaosema usitabiri matokeo ya mechi kwa kuangalia line up ya timu husika au jezi waliyovaa timu B kwa kuwa tu wewe u mshabiki wa timu A.
Nimejifunza kuwa JPM kumbe ni MWANADIPLOMASIA MAHIRI SANA. Mahiri kuliko nilivyomtarajia au kumpima na hata kukadiria namna ambavyo angetekeleza jukumu hilo zito katika mkutano wake wa kwanza wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Muungano wa Afrika (,AU).
Katika mikutano ile niliona namna alivyokuwa anawaleta karibu wageni wake alowaalika katika mikutano hiyo.
You could see his aggressive diplomacy through active talk, locking his eyes into those of the invitee, keeping his hand tight to the invitee”s hand / ands, a beaming and joyus face, endless  friendly gestures to give the invitee a feeling he is home and a friendly host, friendlier body language as well as creating a mood of a long established friendship even though the fact is thats the first or second encounter.
Waingereza walisema Never judge a book by its cover leo nimeithinitisha kauli hii pasina shaka. Naamini hata mabingwa wengine wa diplomasia wameona.
Nakumbuka mwaka jana Nguli wa Tasnia,  Jenerali Ulimwengu aliandika akimtaka Rais JPM atembee walau kidogo kwani akiwa MWANA DIPLOMASIA namba moja wa Tanzania ana nafasi nzuri ya kuwachagiza  viongozi  na hata wawekezaji kuja kuwekeza TANZANIA kuliko anavyoweza kufanya Balozi, Dr MAHIGA.
Uwezo huo wa JPM unaweza kuuona hata alipokuwa na Rais KAGAME wakati wa sherehe ya jengo la Mwalimu  NYERERE.
Balozi, Dr MAHIGA ana nafasi yake lakini Mwanadiplomasia namba moja ana nafasi nzuri na kubwa zaidi.
Viva JPM,
Long live TANZANIA

No comments :

Post a Comment