Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akijibu maswali ya papo kwa papo, bungeni mjini Dodoma Februari 2, 2017.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akimsikiliza Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe wakati
alipouliza swali katika kipindi cha maswali kwa Waziri Mkuu, Bungeni
mjini Dodoma Februari 2, 2017.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
……………………………………………………..
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa
amesema Mheshimiwa Rais, Dkt. John Magufuli hajawahi kutangaza ama kutoa
kauli ya kufutwa kwa vyama vya siasa nchini.
Ametoa kauli hiyo leo (Februari, 2, 2017) Bungeni mjini Dodoma
wakati akijibu swali la Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni,
Mheshimiwa Freeman Mbowe katika kipindi cha maswali kwa Waziri Mkuu.
Katika swali lake Mheshimiwa Mbowe alisema Rais Dkt. Magufuli alinukuliwa akisema atahakikisha anafuta vyama vyama vya upinzani na ifikapo mwaka 2020 hakuna upinzani nchini.
Katika swali lake Mheshimiwa Mbowe alisema Rais Dkt. Magufuli alinukuliwa akisema atahakikisha anafuta vyama vyama vya upinzani na ifikapo mwaka 2020 hakuna upinzani nchini.
Pia Mheshimiwa Mbowe alitaka
kujua nini kauli ya Serikali kuhusu kunyimwa dhamana kwa Mbunge wa
Arusha Mjini, Mheshimiwa Godbless Lema ambaye anashikiliwa kwa muda
miezi mitatu.
Mbali na Mheshimiwa Lema, pia
kiongozi huyo alitaka kujua kuhusiana na kufungwa kwa Mbunge wa
Kilombelo, Mheshimiwa Peter Lijualikali pamoja na madiwani sita wa chama
hicho ambao wamefungwa na viongozi wengine 215 wanakabiliwa na kesi
mbalimbali.
“Kwanza nataka nikanushe kwamba
Mheshimiwa Rais hajawahi kutangaza kuvifuta vyama vya upinzani. Pia
Watanzania wote wanajua nchi hii inaongozwa kwa sheria, kanuni na
taratibu i,” amesema Waziri Mkuu.
Waziri Mkuu ameongeza kuwa
“tunajua katika kuendesha nchi tunaendesha kwa mihimili mitatu ipo
Serikali, Mahakama na Bunge na hakuna mhimili unaoweza kuuingilia
mhimili mwingine,”.
“Pia Watanzania wote wanajua
kwamba jambo lolote ambalo lipo Mahakamani haliwezi kuzungumzwa mahali
pengine popote, hivyo siwezi kutumia nafasi hii kuzungumzia mambo yote
yanayoendelea chini ya sheria na yaliyo mahakamani,” amesema.
Wakati huo huo; Waziri Mkuu
amewahakikishia Watanzania kwamba suala la upungufu wa sukari
halitatokea nchini kwa sababu viwanda vya ndani vinaendelea kuzalisha na
hadi mwishoni mwa Januari vilifikia asilimia 86 ya uzalishaji.
“Hadi kufikia mwishoni mwa msimu
wa uzalishaji ambao ni mwezi Machi, tunaweza kuwa tumefikia malengo na
kama itajitokeza upungufu Serikali itatafuta namna nzuri ya kupata
sukari kwa kushirikiana na wenye viwanda nchini,” amesema.
Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo
wakati akijibu swali la Mbunge wa Mvomero, Mheshimiwa Suleiman Sadiq
aliyetaka kujua hali ya sukari ilivyo nchini kwa sasa na hatua gani
zinazochukuliwa na Serikali ili kunusuru hali ya uhaba wa sukari
isijitokeze.
No comments :
Post a Comment