Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Bwana, Laurean Bwanakunu (kushoto) na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Kibaha Bi.Jenifa Omolo wakibadilishana hati baada ya kusaini makubaliano
ya umilikishwaji wa eneo la ardhi, lenye ukubwa wa mita za mraba
400,000 Dar es Salaam leo, ambayo itatumika kwa ajili ya ujenzi wa
Kiwanda cha kuzalishia dawa na vifaa tiba Kibaha mkoani Pwani.
Muonekano wa chumba cha mkutano wakati wa hafla hiyo ya kutiliana saini. Pichani ni maofisa kutoka Halmshauri ya Kibaha na MSD.
Ofisa Uhusiano Mkuu wa MSD, Etty Kusiluka, akizungumza wakati akimkaribisha Mkurugenzi wa MSD kuzungumza katika hafla hiyo.
Mkutano ukiendelea.
Mkurugenzi
Mkuu wa MSD Bwana Laurean Bwanakunu, akizungumza katika mkutano huo.
Kulia ni Mkurugenzi wa Halmshauri ya Mji wa Kibaha, Bi Jenifa Omolo.
Mkurugenzi wa Halmshauri ya Mji wa Kibaha, Bi Jenifa Omolo (kulia), akizungumza kwenye mkutano huo.
Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Bwana Laurean Bwanakunu (wa pili kushoto) na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Kibaha Bi.Jenifa Omolo (wa pili kulia), wakisaini makubaliano
ya umilikishwaji wa eneo la ardhi, lenye ukubwa wa mita za mraba
400,000 Dar es Salaam leo, ambayo itatumika kwa ajili ya ujenzi wa
Kiwanda cha kuzalishia dawa na vifaa tiba Kibaha mkoani Pwani. Kulia ni
Mwanasheria wa Mji wa Kibaha, Mansuetha Mbena na kushoto ni Mwanasheria
wa MSD, Christopher Kamugisha.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Kibaha, Leonard Mlowe (kulia), akisaini hati hizo za makubaliano.
Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Bwana Laurean Bwanakunu (kushoto) na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Kibaha Bi.Jenifa Omolo wakionesha hati baada ya kusaini makubaliano hayo.
Picha ya pamoja.
Na Dotto Mwaibale
BOHARI
ya Dawa (MSD) pamoja na Halmashauri ya Mji wa Kibaha kwa pamoja leo
wamesaini makubaliano ya umilikishwaji wa eneo la ardhi, lenye ukubwa wa
mita za mraba 400,000 ambayo itatumika kwa ajili ya ujenzi wa Kiwanda
cha kuzalishia dawa na vifaa tiba Kibaha mkoani Pwani.
Hatua
iyo ni Utekelezaji wa mradi wauzalishaji dawa wa ushirikiano wa sekta
ya umma na sekta binafsi yaani PPP, ambapo Mkurugenzi Mkuu wa MSD Bwana,
Laurean Bwanakunu amesema dhamira ya serikali ya viwanda inawezesha
mambo makubwa mawili ambayo ni upatikanaji wa ardhi na kisha kutafuta
masoko.
Amesema
baada ya hatua hii watatangaza zabuni kwa ajili ya kupata wazalishaji
wa dawa na vifaa tiba kama vile maji ya dripu, pamba, gozi na dawa za
maji za watoto ambayo itasaidia kupunguza gharama za kuagiza dawa
kutoka nje ya nchi, ambapo 85% ya awa na vifaa tiba vinaagizwa kutoka
nje ya nchi.
Kwa
mujibu wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Kibaha Bi.Jenifa Omolo
eneo hilo lipo karibuna miundombinu ya reli na barabara hivyo itakuwa ni
hatua ya kuleta maendeleo kwa mji wa Kibaha.
(Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)
(Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)
No comments :
Post a Comment