Nasieku Kisambu Mkurugenzi wa
Mipango Chama cha Wanasheria Wanawake (TAWLA) akizungumza katika
mafunzo ya Haki za Wanawake na Jinsi ya kufanya utetezi katika ngazi ya
Kitaifa, Kikanda na Kimataifa yakiwa na lengo la kuongeza uelewa wa
misingi ya kulinda na kutetea haki za wanawake na watoto Kitaifa ,
Kikanda na Kimataifa.
Kuelewa mifano iliyopo katika
Kanda, Kikanda na kimataifa inayolinda haki za wanawake , Haya ni
mafunzo yanayolenga kujenga uwezo wa Taasisi zinazotetea haki za
wanawake kutumia fursa zilizopo katika mikataba, Taasisi na mifumo ili
kuweza kubadilisha sera na sheria kandamizi na kutetea haki za wanawake.
Mafunzo hayo yanayofanyika kwenye
hoteli ya Courtyard Upanga jijini Dar es salaam yameandaliwa na Chama
cha Wanasheria Wanawake Tanzania (TAWLA) na kwa ushirikiano na mashirika
mengine yanayotetea haki za wanawake na watoto ambapo wadau mbalimbali
kutoka katika taasisi hizo wameshiriki katika mafunzo hayo
Maria Matui Makamu Mwenyekiti wa
Chama cha Wanawake Wanasheria Tanzania (TAWLA) akifungua mafunzo hayo ya
siku mbili yanayofanyika kwenye hoteli ya Courtyard Upanga jijini Dar
es salaam.
Mkufunzi wa Mafunzo hayo Dk.
Clemence Mashamba akitoa mada wakati wa mafunzo hayo yanayoendelea
kwenye hoteli ya Courtyard Upanga jijini Dar es salaam.
Christina Kamili Mkurugenzi
Mtedaji wa Shirika la Tanzania Network Of Legal And Providers
akifuatilia mada iliyokuwa ikitolewa na Mkufunzo wa Mafunzo hayo Dk.
Clemence Mashamba hayupo pichani.
Baadhi ya washiriki mbalimbali wa mafunzo hayo wakifuatilia mada zilizokuwa kititolewa na mkufunzi huyo.
Christina Kamili Mkurugenzi
Mtedaji wa Shirika la Tanzania Network Of Legal And Providers
akifuatilia mada iliyokuwa ikitolewa na Mkufunzo wa Mafunzo hayo Dk.
Clemence Mashamba hayupo pichani.
Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo wakifuatilia mada mbalimbali katika mafunzo hayo.
Mkufunzi wa mafunzo hayo Dk
Clemence Mashamba akiwa na Dotto Joseph Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya
National Oganization For Legal Assistance (Nola)
Maria Matui Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Wanawake Wanasheria Tanzania TAWLA akipitia nyaraka za mmbalimbali za mafunzo hayo.
Washiriki wa Mafunzo hayo wakiwa katika picha ya pamoja.
No comments :
Post a Comment