Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho
Gambo (katikati) akizungumza na vikundi vya wanawake na vijana kutoka
katika Jiji la Arusha kabla ya Kukabidhi hundi za Mikopo ya robo ya
kwanza na ya Pili kwa mwaka wa Fedha 2016/2017.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho
Gambo(Katikati) akikabidhi hundi ya Tsh Mil 425 kwa wawakilishi wa
Wanawake Bi. Mariamu Okash(Kata ya Kati) na Rose Charles(Kata ya
Olorieni).
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho
Gambo akikabidhi hundi ya Tsh Mil 199 kwa wawakilishi wa Vijana Amos
Kosani (Daraja II) na Janeth Prosper (Kata ya Unga Ltd).
Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Arusha
Gaston Gasana (kwanza kulia) akitoa taarifa fupi ya Utoaji wa Mikopo ya
Wananwake na Vijana kwa robo ya kwanza na ya Pili kwa mwaka wa Fedha
2016/2017 kwenye hafla ya kukabidhi hundi za mikopo hiyo.
Mkuu wa Wilaya ya Arusha Gabriel
Daqarro(Kwanza kushoto) akimkaribisha Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho
Gambo kukuabidhi hundi kwa vikundi vya Wanawake na Vijana wa Jiji la
Arusha.
Vikundi vya Wanawake na Vijana
kutoka Kata mbalimbali za Jiji la Arusha wakimskiliza Mkuu wa Mkoa wa
Arusha Mrisho Gambo (hayupo Pichani) kabla ya kukabidhiwa Mikopo
inayotokana na asilimia kumi ya mapato ya ndani.
………..
Nteghenjwa Hosseah, Arusha
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho
Mashaka Gambo amefungua mafunzo ya ujasiriamali kwa vikundi
vinavyokopeshwa na kutoa mikopo kwa vikundi 85 vya wanawake na vikundi
40 vya vijana kutoka katika kata zote za Jiji la Arusha.
Akikabidhi hundi zenye thamani
ya Sh Mil 624 kwa vikundi hivyo ikiwa ni mikopo ya robo ya kwanza na ya
pili kwa mwaka wa fedha 2016/2017 Mhe. Gambo amewataka kinamama na
vijana kutumia fedha hizo kwa shughuli zilizokusudiwa ili ziweze kuleta
manufaa na kuwatoa katika lindi la umasikini.
“Mikopo hii inatolewa ili
kuendeleza shughuli za kijasiriamali ambazo ndizo zilizopelekea mkidhi
vigezo vya kupata Fedha; Nimatumaini yangu fedha hizi zitawawezesha
kuongeza mitaji yenu na kuwapa ari ya kujituma zaidi huku mkizingatia
nidhamu ya pesa ili muweze kuzirejesha kwa wakati na makundi mengine
waweze kupata fedha hizo”Alisema Rc Gambo.
Aliongeza kuwa tofauti na
mikopo hii ya halmashauri baada ya kuwawezesha vijana waendesha boda
boda kwa kuwapatia Pikipiki 200 kundi litakalofuata ni wakinamama ambao
watanufaika na Fedha zitakazorejeshwa na vijana hao kwa kupewa mitaji
midogomidogo kadiri ya uhitaji.
Aidha Rc Gambo alimuagiza
Mkurugenzi wa Jiji kuunda timu maalumu ya kuchunguza utoaji wa Mikopo
kwa Kipindi cha Miaka mitatu kama ilifuata taratibu, vikundi
vilivyonufaika kama ni hai na hali ya urejeshaji.
Naye Mstahiki Meya wa Jiji la
Arusha Mhe. Kalisti Lazaro Bukhay ambaye alishiriki katika zoezi la
utoaji mafunzo na kukabidhi hundi amesema Kikundi ambacho hakitarejesha
fedha zote za mkopo ama kuchelewesha marejesho kwa namna yeyote ile
hakitapatiwa mkopo katika mwaka unaofuata ila wale watakaofanya vizuri
katika biashara zao na kukuza mitaji wataongezewa kiasi cha kukopa
kulingana na hali ya shughuli zao.
Mikopo hiyo inayotolewa kwa
mujibu wa Sheria na miongozo inayoelekeza asilimia kumi ya Mapato ya
ndani ya Halmashauri kutolewe kama Mikopo ya riba nafuu kwa vikundi vya
wananwake na vijana na kwa jiji la Arusha kiasi kinachotakiwa kutolewa
ni Bil 1.2 kwa Mwaka huu wa Fedha hivyo kiasi kilichotolewa ni kwa
kipindi cha nusu mwaka.
Fedha hizo zinatolewe kwenye
Saccos au Vicoba vyenye nguvu katika Kata husika ili kurahisisha
usimamizi na urejeshaji wa mikopo hiyo. Hivyo Saccos na Vicoba ndizo
zinazokopesha vikundi vilivyoainishwa na Kamati ya Maendeleo ya Kata
(WDC) kwa riba ya asilimia 10 na wao hubaki na asilimia 8 kwa ajili ya
shughuli za uendeshaji na kurejesha Halmashauri riba ya asilimia 2 tu.
No comments :
Post a Comment