Mwenyekiti wa Klabu ya Golf
ya Lugalo Brigedia Jenerali Mstaafu Michael Luwongo wakati akizungumza
na Waandishi wa habari Klabuni Jijini Dar es Salaam.
…………………………………………………………………….
Na Luteni Selemani Semunyu JWTZ
Rais
Mstaafu DR. Jakaya Mrisho Kikwete anatarajiwa kuwa mgeni Rasmi katika
mashindano ya kuadhimisha Miaka 10 ya Klabu ya Golf ya Jeshi la Ulinzi
la Wananchi ya Lugalo.
Hayo yamesemwa leo na Mwenyekiti wa Klabu ya Golf
ya Lugalo Brigedia Jenerali Mstaafu Michael Luwongo wakati akizungumza
na Waandishi wa habari Klabuni Jijini Dar es Salaam.
Aliongeza
kuwa Rais wa Awamu ya Nne yeye ndio aliezindua uwanja huu, hivyo ni
fursa nzuri kujionea maendeleo yaliyofikwa katika kipindi cha Miaka 10.
“Uongozi
umeona ni busara kumualika kama mgeni rasmi katika kutimiza miaka kumi
pia ni fursa yeye kuanza kucheza na Mbali na mgeni rasmi viongozi
mbalimbali wa kitaifa na kimataifa wamealikwa kushiriki katika ufunguzi
na ufungaji wa mashindano haya “ Alisema Brigedia Jenerali Luwongo.
Mashindano
haya yatafanyika kwa siku tatu katika viwanja vya Lugalo Gofu Lugalo,
kuanzia tarehe 17 hadi 19 februari 2017 ambapo Wataanza wachezaji wa
kulipwa (Pros) na wachezaji wasaidizi (Caddies).
Aliongeza
kuwa Siku ya pili ya tarehe 18 Februari, watashindanishwa wachezaji wa
Ridhaa (Armatures) na siku ya tatu yani tarehe 19 Februari,
watashindanishwa wachezaji waliofanya vizuri tarehe 18 februari
ikifuatiwa na sherehe za ufungaji wa mashindano hayo.
Brigedia
Jenerali Mstaafu Luwongo alifafanua wakati klabu inazinduliwa ilikuwa
na mashimo Tisa tu ya mchezo huu (9 Holes), lakini kwa sasa imefanikiwa
kuwa na mashimo kumi na nane (18 Holes) kama mchezo huu unavyohitaji.
Kwa
upande wake Nahodha wa Klabu ya Lugalo Kapteni Japhet Masai alisema
kutokanana na kuwa mashindano makubwa sheria za ndani zimeandaliwa
ambazo hazitapingana na Sheria za Kimataifa.
“
Wachezaji watambue kuwa tutafuata Mwongozo wa Kimataifa wa kuendeshha
mashindano ili kuwa na sifa za kimataifa na kuiletea sifa nchi katika
uandaaji wa mashindano yenye viwango” alisema Kapteni Masai.
Kwa Upande wake Mmoja wa Wadhamini wa Michuano hiyo kutoka kampuni ya Bima ya Resolution Kaimu Meneja wa Masoko Marcellino Mitawa alisema wameamua kuongeza nguvu katika golf ili kuondoa dhana kuwa ni mchezo wa matajiri.
No comments :
Post a Comment