Friday, December 2, 2016

UKAGUZI WA MAENDELEO YA SEKTA YA ARDHI KATIKA MKOA WA KATAVI

wapi
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt.Angelina Mabula (kulia) akikagua nyumba za mradi wa makazi zinazojengwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) wilayani Mlele mkoani Katavi. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Mpanda bibi Lilian Matingana, katikati yao ni Meneja wa NHC mkoani KataviBw. George Magembe. 

wapi-1
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angelina Mabula akizungumza na wananchi wa Wilaya ya Mlele mara baada ya kusikiliza kero na matatizo yao kuhusu sekta ya ardhi. Dkt. Mabula amemaliza ziara ya siku mbili mkoani Katavi na ameeleke amkoani Rukwa.

wapi-2
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angelina Mabula (kushoto) akitoa maelekezo kwa karani wa Baraza la Ardhi na Nyumba la Wilaya –Mpanda, namna bora ya utunzaji kumbukumbu za majalada ya mashauri wakati alipotembelea Baraza hilo ili kufuatilia utendaji kazi wake.

wapi-3
Meneja wa Shirika la Nyumba la Taifa Mkoa wa Katavi Bw. George Magembe akitoa maelezo ya miradi mbalimbali ya ujenzi wa majengo ya makazi na biashara inayotekelezwa na Shirika mkoani Katavi wilayani Mpanda kwa Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angelina Mabula

wapi-4
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angelina Mabula (aliyesimama) akizungumza na wananchi wa Kata ya Kazima katika Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda mkoani Katavi mara baada ya kusikiliza kero wanazokumbana nazo wanapohitaji huduma za sekta ya ardhi. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Bibi Lilian Matinga na kulia kwa Dkt. Mabula ni Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda Bw. Willy Mbogo.
wapi-5
Mkazi wa  Kata  ya Nsemulwa katika Halmashauri ya Manispaa ya Wilaya ya Mpanda mkoani Katavi Bibi Maria akieleza tatizo alilo nalo kuhusu huduma za ardhi mbela ya Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt.  Angelina  Mabula.

wapi-6
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi  Dkt. Angelina Mabula (kushoto) akizungumza na wananchi wa Kata ya Nsemulwa mkoani Katavi mara baada ya kusikiliza matatizo yao kuhusu huduma za sekta.
………………………..
Serikali imeagiza Halmashauri zote nchini kutokuchua ardhi ya mtu bila ya kulipa fidia wakati wa kutwaa maeneo kwa ajili ya mpango wa matumizi mbalimbali.

Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi DKT. Angelina Mabula amesema hayo wakati wa ziara ya kiazi mkoani Katavi wakati alipotembelea kwa lengo la kukagua utoaji huduma za sekta ya ardhi unavyofanyika pamoja na kukagua shughuli mbalimbali.

Amesema Serikali ilikwishatoa maealekezo hayo ya kuzingatia Sheria ya Ardhi ya mwaka 1999 iliyofayiwa mabadiliko baadaye ambayo inatoa haki ya mtu kulipwa fidia ya ardhi tupu na maendelezo yake pindi ardhi yake inapotwaliwa.

“unapopima maeneo kulingana na miji inavyokua mikubwa ama inavyotanuka, lazima kwanza fidia ilipwe  kwa mtu anayekutwa pale ndipo wapishe katika maeneo yao, na iwapo mtu huyo analo eneo kubwa linalobaki pia alipwe  fidia kwa mujibu wa sharia,”alisema Dkt. Mabula.

Alisisitiza pia lazima kipaumbele cha umilikishaji wa kiwanja kitolewe kwa mtu ambaye eneo lake limechukuliwa badala ya kumilikisha watu wengine wenye uwezo waki fedha.
Amesema kwamba iwapo kutakuwa na uhamishowa watu wakati wa utwaaji ardhi basi uwe ni kwa ajii ya kupisha huduma za msingi za jamiik ama vile ujenzi wa shule, hospitali, barabara ama Mahakama na vitu vingine vinavyofanana na hivyo.
Naibu Waziri huyo wa Ardhi ataendelea na ziara yake ya kukagua utendaji wa sekta ya ardhi katika mikoa ya Rukwa, Songwe na Mbeya

No comments :

Post a Comment