Meneja wa Mradi wa ujenzi wa
Kiwanja cha Ndege cha kisasa cha Julius Nyerere (JNIA), Mhandisi
Mwanaidi Mkwizu (wa kwanza kulia) akitoa muhtasari wa maendeleo ya mradi
huo mbele ya timu ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo kutoka Tume ya
Mipango pamoja na wajumbe kutoka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano wakati wa ziara ya ukaguzi wa mradi huo.
Meneja mradi wa ujenzi wa kiwanja
cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), Mhandisi Mwanaidi
Mkwizu (aliyevaa suti) akitoa melezo kwa Timu ya ukaguzi wa Miradi ya
Maendeleo kutoka Tume ya Mipango.
Timu ya ukaguzi wa Miradi ya Maendeo ikiendelea na ukaguzi wa maendeleo ya mradi huo ndani ya jengo la abiria.
Mwonekano wa sehemu ya mbele wa Jengo jipya la abiria katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (Terminal III).
Eneo watakapopita abiria kutoka ndani ya jengo la abiria wakielekea kupanda ndege.
Moja ya sehemu za ndani ya jengo la abiria.
Sehemu ya ujenzi unaoendelea katika mradi huo.
Mhandisi Omari Athuman (mwenye
kofia ya bluu) akiangalia kazi ya kuunganisha mitambo ya moja ya
majenereta ya kisasa kwa ajili ya dharura ya umeme katika uwanja huo.
Majenereta ya kisasa kwa ajili ya dharura ya umeme katika kiwanja hicho.
……………
Tume ya mipango imefanya ziara
katika mradi wa ujenzi wa jengo la III la abiria katika uwanja wa Ndege
wa Julius Nyerere (Terminal III) jijini Dar es Salaam kwa lengo la
kukagua maendeleo ya mradi huo na kuelezwa kuwa ujenzi umefikia asilimia
65.
Akitoa maelezo mbele ya timu ya
wataalamu kutoka Tume ya Mipango, Meneja wa Mradi huo Mhandisi Mwanaidi
Mkwizu alieleza kuwa ujenzi huo unaotekelezwa na Mkandarasi wa kampuni
ya BAM kutoka Uholanzi ulioanza Juni 2013 na unatarajiwa kukamilika
ifikapo mwezi Desemba Mwaka 2017.
Akielezea miundombinu ya uwanja
huo, Mhandisi Mkwizu alisema kuwa uwanja huo wa kisasa una barabara ya
kuruka ndege (runway) yenye urefu wa kilometa 3 na upana wa mita 60
ambapo upana unaohitajika kwa matumizi ya ndege ni mita 45.
Aliongeza kuwa mradi huo pia
umeangalia changamoto ya kukatika umeme mara kwa mara na kuamua kutafua
vyanzo mbalimbali ili kuondokana na utegemezi wa chanzo kimoja ambacho
kinaweza kukwamisha shughuli katika uwanja huo pale inapotokea hitilafu.
Alieleza kuwa kutakuwa na njia
mbili tofauti za kuleta umeme kutoka TANESCO ambapo njia moja ni kwa
ajili ya dharura na pia endapo kutakuwa na tatizo la kukatika umeme
kupitia njia za TANESCO, umeme utapatikana kutoka chanzo mbadala cha
dharura kwa kutumia jenerata nne kubwa za kisasa za dizeli zilizopo eneo
la mradi ambazo zinatosha kukidhi mahitaji ya eneo hilo.
Alisisitiza kuwa tayari wamefanya
mazungumzo na TANESCO na kukubaliana kuwa njia hizo za umeme ni kwa
ajili ya uwanja huo pekee na hakuna wateja wengine watakaounganishiwa
katika njia hizo.
Mhandisi mkwizu alimalizia kwa
kusema kuwa yeye pamoja na timu yake ya wataalamu wanaendelea kufanya
usimamizi wa karibu ili kuhakikisha kuwa utekelezaji wa mradi huo
unaenda sambamba na malengo yaliyopangwa.
Wataalamu wa ukaguzi wa miradi
kutoka Tume ya Mipango walipata fursa ya kutembelea maeneo mbalimbali ya
ujenzi wa mradi huo na kuonesha kuridhishwa na kasi yautekelezaji huku
wakimshauri menejea wa mradi huo kuendelea na ufanisi wake katika
kusimamia kazi hiyo ili kuhakikisha malengo ya mradi huo yanafikiwa.
________________
Adili Justine Mhina,
Information Officer,
Information Officer,
Ministry of Finance and Planning,
Planning Commission,
Box 9242,
Dar es Salaam.
Tel 2112681-4/2127122
Fax 2115519/2117103
Mob 255-787 677 881
Box 9242,
Dar es Salaam.
Tel 2112681-4/2127122
Fax 2115519/2117103
Mob 255-787 677 881
No comments :
Post a Comment